Curtis James
Jackson III , kwa jina maarufu 50CENT ni
mjasiriamali wa kuheshimika huko Marekani na duniani kwa ujumla. Mbali
na
Muziki, ambapo wimbo wake wa In Da Club, ulimpatia jina kubwa kwa mara
ya
kwanza na kuongoza kundi na label ya GUNIT, mwanamuziki huyo wa miondoko
ya RAP, anamiliki makampuni ya biashara
nje ya hata Muziki. Makala hii inakupa dondoo ya baadhi ya mambo
makubwa aliyokwisha fanya na pia ushauri wake 50CENT kwa wajasiriamali
wengine.
Kwa sasa 50 Cent anamiliki kampuni ya SK Energy
inayotengeneza kinywaji maarufu cha kuleta nguvu ya mwili kiitwacho SK Energy.
Fuatilia kampuni ya SK Energy kwa kubofya hapa.
Mbali ya hivyo , 5OCENT anamiliki kampuni ya mambo ya Teknolojia ambapo yeye
mwenyewe ndie mkurugenzi muendeshaji. Kampuni hiyo ya Teknolojia inaitwa SMS
AUDIO. Kampuni hii ya Teknolojia aliianzisha mwaka 2011.
Ukiachilia na ukweli kuwa ndiye Afisa Muendeshaji wa SMS AUDIO,
mwanamuziki huyo kwa kutumia uzoefu wake wa muziki, ameshiriki katika kubuni na
kuunda vifaa vya kusikilizia muziki – headphones ambavyo vina ubora wa hali ya
juu. Bofya hapa kutembelea website ya SMS AUDIO.
50CENT pia anamiliki kampuni ya kutengeneza movie, na kutengeneza Games.
Ukiachilia umiliki wa makampuni yake binafsi ya kuzalisha
bidhaa, 50CENT ameshawahi kufanya mkataba na Reebook kutengeneza raba, amewahi
pia kufanya mkataba wa kutengeneza uturi
(spray).
Alipohojiwa website maarufu ya FORBES, kuhusu siri ya
mafanikio yake katika muziki na biashara, 50CENT alisema ni kujitoa kwa nguvu zote katika kufanya kazi
kwa ajili ya watu. Anasema 50CENT kuwa bidhaa inayotolewa na mjasiriamali ni
zao la mwisho la kujitoa kwa mjasiriamali husika, hivyo kila anapouza bidhaa
anauza nguvu au uzoefu wake katika jambo husika.
Na zaidi ya yote, uwezo wa
kufanya jambo bila kuogopa hasara, kufanya jambo kwa nadharia kuwa hakuna cha
kupoteza.
Sikiliza na kuangalia video hii yenye kukudokeza uwekezaji
mkubwa katika ujasiriamali uliofanywa na 50CENT.
0 comments:
Post a Comment