KARMA INAVYOATHIRI MAISHA YAKO

Kwa mujibu wa  dhana ya KARMA, mengi yanayomtokea binadamu ni  matokeo ya matendo yake binadamu huyo. Yaani ukitenda mema, mazuri yanakuja, na ukitenda mabaya, mabaya yanakuja.  Pia ikumbukwe kuwa matokeo ya mazuri au mabaya si lazima yaje muda mfupi toka tukio litokee. Mtu hupata ‘faida’ ya matendo  kwa nyakati tofauti , saa nyingine matokeo yanaweza kuwa ni ya haraka, na wakati mwingine si ya haraka. Chukulia mfano ufuatao:

Kijana JM, baada ya kumaliza darasa la saba na kutofaulu alipelekwa shule ya sekondari  ya kulipia ambako hakupenda pia hata kusoma. Alikuwa kiongozi wa shughuli zote zenye kuvunja maadili. Na matokeo yake form 4 yalipotoka, alijikuta akiambulia divisheni ‘ziro’. Hata hivyo kwa kuwa mzazi wake JM alikuwa ana uwezo wa kifedha, JM alipelekwa kujiendeleza kwenye kozi fupi fupi za kiingereza na kompyuta, na baadae mzazi wake akamuajiri kwenye kampuni yake kama msamimizi wa stoo.   

Hata hivyo JM hakuridhika na mapato aliyokuwa akipata toka katika kazi yake hivyo akafanya mpango wa kwa kushirikiana na rafiki zake ambao huwa ‘anajirusha’ nao ili waibe mali za baba yake.Katika moja ya hatua za wizi huo, ilibidi wavamie ofisi ya baba yake JM usiku , na JM alikuwa kiongozi wa uvamizi huo. Hata hivyo katika pilika za uvamizi huo, JM alijikuta akipigwa risasi na mlinzi wa kampuni , katika harakazi  za uvamizi huo. Kijana JM alijeruhiwa vibaya , na alifariki mara tuu baada ya kufika hospitalini. Majirani na watu wengi waliolizungumzia tukio  walisema eti JM alipata ‘Adhabu’ yake kutokana na kumkaidi baba yake.

Mfano hapo juu wa kijana JM, unaonyesha jinsi ambavyo mfululizo wa matendo ya JM ulivyochangia katika kufikisha hatima yake ya kifo , na matokeo mengine madogo madogo kabla ya kifo chake kama vile kufeli mitihani, kama vile kutokuridhika na kipato alichokuwa anapata toka kwa mzazi wake.

Kwahiyo basi, sio kwamba kwa kuwa unafanya mabaya na bado hauoni madhara ya mabaya uyafanyo haimaanishi kuwa madhara kwako hayaji, yatakuja tuu, iwe moja kwa moja au hata kwa njia tofauti ya kukuumiza. 
Na pia kama watenda mema , ila hauoni mafanikio ya haraka , usikate tamaa, mafanikio yaja, iwe kwa haraka, baadae sana, mafanikio ya moja kwa moja au kwa jinsi ambayo haujaitegemea ila mafanikio yatakuja tuu. 
Hiyo ndiyo KARMA.

Kwa maelezo zaidi kuhusu KARMA, jisomee makala ifuatayo hapa chini:

DOUG CASEY ON KARMA 
Share:

1 comment:

  1. Kweli kabisa utichokipanda ndio utakachokivuna, vile.mchimba kisima huingia mwenyewe

    ReplyDelete