Kwa watu wengi , mpango wa kuishi nje ya nchi una maana ya
‘Kuzamia’. Yawezekana neno kuzamia linatumika sivyo ndivyo kwani asili yake ilikuwa
haswa miaka ya nyuma sana , ambapo wengi walienda nje ya Tanzania kwa kupitia meli ambapo
walijificha baada ya kuzamia meli, na kuondoka na meli husika mpaka huko
ughaibuni ambako wakifika huko hujichanganya na wenyeji na kuanza ‘kutafuta’
maisha.
Pengine mtindo huu wa kuenda ughaibuni kwa kuzamia meli unatumika bado
ila haujashamiri sana siku za hivi karibuni.
Badala ya kuondoka kwa mtindo huu wa kuzamia meli ambapo
wazamiaji hao hawakuwa na hata vibali halali vya kuingia nchi husika, achilia
mbali kuwa na hata Passport ya Tanzania, siku hizi, wabongo hawatumii meli
kuzamia, ‘wazamiaji’ wengi wa siku hizi
huwa na vibali halali vya kusafiria na hata kupanda ndege au mabasi halali
kabisa na kuingia nchi husika hata hivyo wanapofika huko hupitiliza muda halali
wa kukaa huko nchi husika, na hivyo hiyo kuonekana kama na wao ‘walizamia’.
Kwahiyo neno kuzamia siku hizi halitumiki kama zamani
kueleza taswira ya aina ya usafiri mtu aliotumia kusafiria – yaani kuzamia
meli, badala yake neno kuzamia limekumbwa na utata wa maana tofauti. Kwa
wengine neno ‘kuzamia’ linamaanisha aina yoyote ile ya kuishi ughaibuni zaidi
ya shughuli halali iliyompeleka mtu kwa mara ya kwanza.
Katika maana hii ya pili , kuna mgongano mwingine wa maana
ya kuzamia. Je, wewe unaonaje:
1. Je kila
mtu anayeishi ughaibuni zaidi ya shughuli yake ya awali iliyompeleka huko ni
mzamiaji hata kama anacho kibali halali cha kuishi huko ?
2. Au mzamiaji ni yule mbongo anayeishi ughaibuni pasipo kuwa na
kibali halali cha kuishi huko ughaibuni ?
Mhhhhhhhh, pagumu hapo mkuuu
ReplyDelete