Kila
kukicha tunaona mitandaoni au mitaani watu wakizungumzia 'kula bata'.
Je, ni kweli kula bata ndio uthibitisho wa mafanikio ya kimaisha ? Je,
kula bata ni sawa na kupumzika na kuburudika ? Je, ni kweli kuna maana
tofauti za kula bata ?
Msikilize kijana huyu wa kibongo akielezea jinsi alivyo na maendeleo na anavyo kula bata !
“Mie, aah we acha kabisa, Mungu kanijalia neema, nina
laptop, nina blackberry, nina badilisha club ninavyotaka, hizo Lounge ndio
usiseme sijui Savannah, Nyumbani Lounge , huko kote mie nyumbani.
Yaani mademu
wanavyo ni shobokea, halafu mie hata si wamandai, nimepoa zangu na mademu
watatu tuu.
Yaani swaga ninazotoa Facebook, nina rafiki kibao, nakaribia
kufikisha elfu nne. Mie si mkali bwana.
Dunia hii raha ujipe mwenyewe. Nijipe shida ya nini, wakati
nakaa kwa wazee (wazazi), halafu naingiza kitu kama elfu ishirini kila siku.
Kwani nikitumia elfu 15 kwa siku, ikabaki
5 inalinda mfuko, hata ikibaki buku ya vocha poa tuu, kuna shida gani?. Hela utumiavyo, ndivyo zinavyokuzoea”.
Kama kujipa raha kwenyewe ndio hivi, basi kazi ipo ! Maisha
bora kwa kila mtanzania kweli yanawezekana!
Nimefika hapa kupata maanaya "kula bata" lakini naona maswali tu.
ReplyDeleteNimefika hapa kupata maanaya "kula bata" lakini naona maswali tu.
ReplyDelete