Njia ya haraka ya kuvuta bahati ni kutumia bahati ambazo tayari unazo ila haujazitambua na hivyo haujaziweka katika mchakato wa kuzifanya zikuletee mafanikio.
Mara nyingi tunawaza sana vile tusivyo navyo , badala ya kuwaza tulivyo navyo. Mfano, unaweza sema huna hela ya kujilipia chuo ili ujifunze ujuzi fulani, lakini MB hazikuishii ili uweze kuwepo mtandaoni na kupost selfies zako au kudownload videos mbalimbali za burudani wakati ungeweza kutumia mtandao kufanya mambo mengi.
Unalalamika hauna network ya kukusaidia wakati una marafiki kibao pengine wa chuoni, au wa kukutana nao tuu mtandaoni ambao wangeweza kukusaidia, ila namna ulivyojitengeneza mtandaoni kwa aina ya posts zako , wengi wanaogopa kuwa karibu nawe kwa mambo "serious".
ili bahati ilete maana katika maisha yako ni lazima uwe umejiandaa kuitumia bahati husika, na hata ikiwepo ni lazima ufanye kazi kuilinda. Ndio maana wapo watoto wa matajiri wanakuja kuishi maisha ya kifukara, wapo waliobahatika kuwa watu maarufu ila wameshindwa kuutumia umaarufu wao kujiletea maendeleo.
--Tafakari , chukua hatua
0 comments:
Post a Comment