Faida za WhatsApp , Facebook, Instagram au mitandao mingine ya kijamii unazijua
? Au kufupisha habari je, wewe unanufaika na hii mitandao ya kijamii ? Kutana na bwana M, ambaye anadai kwake faida
kubwa ya mitandao hii ni kuwa inamfanya asijione mpweke. Ni sehemu
ya burudani na kufahamu nini kinaendelea katika ulimwengu unaomzunguka.
Anachozungumzia bwana M ni kuwa mitandao
ya kijamii kama WhatsApp , Facebook , na Instagram inawapa watu wengi
uwezo wa kujielezea yale ambayo pengine katika mazingira waliyopo wanashindwa
kujieleza.
Athari za Uhuru wa kujieleza ndani ya WhatsApp, Facebook , Instagram
Hata hivyo hapo katika kujielezea ndipo kunapoweza leta matatizo badala
ya kumsaidia mtumiaji wa mtandao. Nazungumzia pale ambapo mtu badala ya kukaa
chini na mhusika na kumueleza malalamiko yako, wewe unatoka na kuenda kutangaza
matatizo yako au kutoridhika kwako au hasira zako huko mtandaoni.
Status/Posts za WhatsApp, Facebook, Instagram zinasema mengi
Kuna watu unaweza jua mood zao
kupitia status wanazoweka. Kwa yule ambayo amekukosea au mliye katika
mfarakano, yeye hatojisikia vizuri hata kidogo, na huko unapoenda kutangaza
wala hakuna wa kukusaidia.
Tafsiri ya posts zako za WhatsApp, Facebook, Instagram
Jambo lingine la kukumbuka ni kuwa
kama unapopost malalamiko, kashfa au kejeli kwa kuwa umekasirishwa au unahisi
kuonewa na mtu fulani , unajijengea picha mbaya kwa baadhi ya watu kuwa wewe si
mzuri katika mahusiano ya mtu na mtu, hivyo watu wakae mbali nawe , kwani hujui
namna ya kumaliza matatizo kati yako na watu unaohusiana nao, badala yake
unakimbilia mtandaoni.
Athari zake
Unapojionyesha kuwa hauna uwezo wa
kumaliza matatizo yako bila kuenda mtandaoni , unajiweka katika mazingira
magumu mfano ya kupata kazi, au kupata washirika wa kufanya nao dili za biashara
n.k kwakuwa wataogopa kuaibishwa mtandaoni.
Pia kujizoesha kukimbilia mtandaoni
kutangaza matatizo yako badala ya kutafuta njia ya kuyamaliza huko pembeni ,
kunadhoofisha uwezo wako wa kujenga mahusiano bora.
Hitimisho
Pamoja na umuhimu wa mitandao ya
jamii ya kutuweka karibu na watu wengi, tusisahau kujenga mahusiano ya mtu
mmoja mmoja. Na lolote linalotokea baina yako na mtu au kundi fulani huko nje
ya mitandao ya kijamii, jitahidi ulimalize huko huko nje, na sio kulipeleka
mtandaoni kana kwamba huko mtandaoni kuna majaji wa kukupatia haki.
Kusoma namna unavyoweza kutumia mtandao kujinufaisha, cheki hii post , bofya HAPA
Kusoma namna unavyoweza kutumia mtandao kujinufaisha, cheki hii post , bofya HAPA
0 comments:
Post a Comment