Tafakari yetu leo inahusu HATERS (Wale unaoamini
wanakuchukia).
Unaamini kuna watu wanakuchukia kwakuwa unadhani wanakutakia
mabaya, unaamini hawakupendi na wanamipango ya kukurudisha nyuma. Hawapendi
furaha yako, na wanasubiria tuu uanguke. Unawachukie na pengine umeshaandika
status maalum juu yao hapa FB, au upo njiani zikikupanda siku unawapa “makavu”
live kwa kuchafua wall yako.
Ndio, unastahili kuwakasirikia, unastahili kutokufurahia
wayafanyayo na unastahili kujipanga ili haters wasifanikiwe wanachofikiria juu
yako. Ila leo nataka kukukumbusha hater mmoja aliyejificha na anayeweza
kukumaliza kwa uharaka kwa kuwa pengine haujamshtukia. Hater huyo ni wewe
mwenyewe kwakuwa:-
Kuna mambo ya msingi unatakiwa uyafanye ila umekuwa mtu wa
kutafuta visingizio usikamilishe hayo mambo ya msingi. Kwa mtindo huu unafanana
na haters kwani unajikosesha fursa wewe mwenyewe. Acha visingizio , jitume kweli kwa hicho ulicho
nacho, kwa mazingira uliyo nayo.
Wewe
pengine umekuwa ukiwafanyia wengine ubaya au visa, pengine si kwa chuki ila
unafanya hivyo ukiamini ni haki yako ili ufanikiwe. Matokeo yake ni kuwa
unajijengea chuki na uadui kwa wengine. Unajikosesha uaminifu hivyo kujiharibia
wewe mwenyewe kama hao haters wanavyotamani kukuharibia.
Hauamini
katika uwajibikaji ili kusaidia jamii. Unadhani la msingi ni bora wewe upate ,
mkono uende kinywani. Hata hivyo kwa utendaji wako mbovu, kwa kutokuwajibika
kwako iwe kielimu , kibiashara , kimalezi n.k jamii yetu inaporomoka siku hadi
siku. Haulioni hili kama ni janga litakalokuja kuumiza wewe mwenyewe pia. Na
cha ajabu upo makini kulaumu wengine kuhusu maisha magumu na mporomoko wa
maadili na hali ya kiuchumi.
Ok, wakati
unaweka mikakati ya kupambana na haters, weka pia mkakati wa kuwa mtu bora
zaidi kila siku, ili upunguze madhara unayojijengea siku hadi siku kwa maisha
yako mwenyewe.
Nikuache na msemo huu toka kwa William Faulkner:
“Unless you're ashamed of yourself now and then, you're not honest”" Isipokuwa tuu unajisikia nyakati fulani fulani aibu kuhusu wewe mwenyewe, jua haupo mkweli".
0 comments:
Post a Comment