Hivi leo ukiwa na kama Tshs. LAKI MOJA ya bure bure hivi, utaamka hapo ulipo na kuanza tuu kuitumia bila mpangilio , mara umenunua hiki, mara kile hata kama sio cha msingi. Kati hiyo laki yako ukaamua kwenda chooni na kudumbukiza “msimbazi” –elf10 kwenye tundu la choo?
Bila shaka jibu ni HAPANA. Lakini embu tafakari kidogo namnatunavyotumia MUDA ambao una thamani kubwa pia, pengine zaidi hata ya LAKI MOJA, utagundua kuna wakati yawezakana unatumia kama huyo jamaa kwenye mfano wa laki moja hapo juu.
1. Je, unao mfumo wa kujua namna gani na kiwango gani cha muda unatumia kwa shughuli zako ? Je, shughuli hizo ambazo zinatumia muda wako zinakuletea manufaa kwako, au ni kama kutupia elf10 chooni ?
2. Ndio unahitaji kupumzika na kuburudika hata hivyo hata kupumzika na kuburudika hakumaanishi kuwa ni "kupoteza muda", bali kupumzika na kuburudika huko pia kuna manufaa yako kiafya, kiakili, na hata kukujenga kimtandao n.k . Je, na huu muda pia umewekewa uthibiti, maana ni kama hiyo lakini moja, ukaamua yote kwenda kununua SODA au BIA na kukaa unywe, wakati kumbe una shida na mahitaji mengine ya hiyo hela. Kutumia sehemu kubwa ya muda wako katika starehe na anasa waweza kufananisha hivyo.
3. Je, unafanyaje kupunguza hasara ya muda unaopotea bila ridhaa yako, kama vile Kwenye foleni ya barabarani, Kwenye ofisi za watu wengine unapoenda kusubiri huduma au kununua kitu ?
4. Je , ni kwa kiwango gani unazuia vitu vinavyoharibu umakini wako katika matumizi ya muda kama vile: kufuatilia vipindi usivyopangilia katika TV, kujikuta ukifanya jambo lingine lisilo katika ratiba yako, au hata mpangilio mbovu wa vitu kiasi kwamba unapoteza muda mwingi kuvipata. Mfano unaamka asubuhi unatumia DK5 kujua mswaki upo wapi, halafu DK10 kutafuta wapi uliweka funguo, dk5 kujua peni ipo wapi !!
Kwa ujuzi zaidi kuhusu matumizi bora ya muda soma makala hizi:-
1. Hii kutoka Business Insider BOFYA HAPA
2. Hii kutoka ENTREPRENUER.COM. BOFYA HAPA
Au cheki video hii toka kwa Dr. Randy Pausch akielezea kwa undani mambo ya Time Management
Mtagulize mgu ktk kila jamboo
ReplyDelete