MBINU YA KIPEKEE YA KUWA MBUNIFU NA MWENYE BUSARA


Fans jumamosi njema.
Tafakari yetu ni kuhusu uwezo wa kufikiri, kubuni na kufanya maamuzi:-
Akili zetu zinafananishwa na mwamvuli ambapo ili mwamvuli ufanye kazi vema wakati wa mvua/jua ni lazima mwamvuli huo uwe umefunguliwa. Ndivyo ilivyo akili zetu zinahitaji kuwa zimefunguliwa ili zifanye kazi vema ya kufikiri, kubuni na kufanya maamuzi vema. Twaweza kufungua akili zetu kwa:- 
Ni kupitia kujifunza mambo mengi ya msingi, kupata uzoefu wa kazi, mazingira na mahusiano tofauti tofauti. Kisha kupitia uzoefu na uelewa mkubwa tulioupata utaweza kuchambua mambo na kufananisha au kutofautisha ili kujua kipi ndio kipi, na yapi ni ya msingi yapi si ya msingi. 
Steve Jobs aliwahi kugusia hili aliposema wale tunaowaona ni wabunifu na wana uwezo mkubwa wa kiakili ukweli ni kwamba hata wao wenyewe wanaona aibu kusema wana uwezo mkubwa kama wanavyofikiriwa kwani kinachotokea ni kuwa wao hawana kipya wanachokiona zaidi ya yale ambayo tayari yapo, ila wao kupitia uzoefu, ufahamu na tafakari ya mambo mengi wanaweza kuona kile ambacho wengi hatuoni.
Na ndio maana hata Albert Einstein tunayeweza kumuita "Jinias", aliwahi sema : “I have no special talents. I am only passionately curious.” 
― Yaani sio kwamba anakipaji fulani haswa maalum bali ni kwa sababu ni mdadisi-yaani anapenda kujua vingi, yaani ubongo wake UMEFUNGUKA.
--Na mgunduzi wa gropu ya umeme na Kamera aitwaye Thomas Edison aliwahi sema: 
"Genius is one percent inspiration and ninety-nine percent perspiration".
Yaani : Kuwa na akili za kipekee kunatokana na 99% ya bidii ya kujituma, na 1% iliyobaki ni kuwa na msukumo.
---Fan wa MBUKE TIMES usitegemee kuona urahisi wa kutatua changamoto zako bila kuwa na ufahamu wa kutosha. Je ni mambo gani unajifunza kila siku? Je yanasaidia kuboresha uwezo wako wa kufikiri, kuamua na kuwa mbunifu?
Jitume leo hii na siku zote, sio lazima uwe kama hao "majiniasi" ila busara, ujuzi na hekima utakayopata kwa kuwa na ufahamu mkubwa itakusaidia wewe na kizazi chako.

Nikuache na quote hii toka kwa Steve Jobs:
"Creativity is just connecting things. When you ask creative people how they did something, they feel a little guilty because they didn't really do it, they just saw something. 
It seemed obvious to them after a while. That's because they were able to connect experiences they've had and synthesize new things."
Na hii toka kwa Thomas Edison:
"Opportunity is missed by most people because it is dressed in overalls and looks like work."

Share:

0 comments:

Post a Comment