MATESO HAYA YA TEMBO WA INDIA NA NINI CHA KUJIFUNZA (VIDEO NA PICHA)

Tembo akiwa amezungushiwa vizuizi. Picha na YouTube video
Nchini India tembo hufugwa pia kama wanyama binafsi kwa shughuli za kubeba mizigo au maonyesho.me
Malezi ya tembo wa aina hiyo yamekuwa gumzo duniani hususani mbinu inayotumika kuwafanya wawe watiifu.
Tafakari yetu leo inahusu MAKUZI na FIKRA ZETU kupitia habari ya kweli ya tembo.
Ipo hivi: tembo wanaofugwa kwa matumizi binafsi kwa nchi kama India na Thailand ili wawe watiifu wanafundishwa toka  wakiwa wadogo kuwa inambidi kukubali kuwa hawezi kujitatua kutoka katika kizuizi alichowekewa. Yaani tembo akiwa mdogo hufungwa katika mti au kitu kizito ambapo baada ya kuhangaika sana kujinasua hujikuta hawezi , na hivyo huacha kabisa juhudi za kujinasua. 
Tembo huyo huendelea na tabia hiyo ya kuacha kutafuta kujinasua hata akiwa mkubwa. Hivyo waweza kukuta tembo kafungwa  kwenye mti au kitu kizito ambacho kwa ukubwa na nguvu ya tembo, akiamua na kufanya juhudi anaweza kujinasua. Hata hivyo kwakuwa keshaaminishwa toka akiwa mdogo kuwa yeyé kama yeyé hana nguvu ya kujinasua, basi hubaki hivyo hivyo.
Binadamu nao wamekuwa wakifanyiwa hivi:
Je, kuna wakati unajihisi tuu kuwa hauwezi kuamua jambo fulani, hauwezi kufanya jambo fulani kwa sababu tuu unahisi haiwezekani. Haujawahi jaribu kufanya tofauti, ila hisia zako zinakuambia hata ukifanya hautofanikiwa. Hali hiyo inaongozwa na uwoga kuwa pengine kuna mkandamizo juu yako utakaotokea ukijaribu kufikiria tofauti, ukijaribu kuwa tofauti. Kwa kifupi jibu kwako linakuwa ni : HAIWEZEKANI kwa namna yoyote HAIWEZEKANI.
Mifano: 
1. Pengine wazazi wamekuwa wakitumia vitisho kwa watoto na kujenga utegemezi ili kuendelea kubaki wa kuogopwa. 
2. Wanandoa na wapenzi wa kawaida nao wamekuwa wakitafuta namna ya kulazimisha utiifu kwa wengine kwa kutumia vitu vinavyoleta utegemezi na kuondoa nguvu za maamuzi ya mwingine kama vile pesa , mali na mambo mengine. Mfano wakuta mtu anashindwa kuamua kwa usahihi mambo ya msingi kwa kuwa tuu ameamini kuwa mumewe au mke wake ni lazima atakuwa sahihi, au hana buni kukubaliana naye kwa kuwa ndiye anayemfanya aishi na kupata apatayo. Ameamini hawezi kufanya mabadiliko mengine yoyote.
3.Tumeaminishwa kuwa mfumo pekee wa elimu utakaomsaidia mtoto ni shule ya msingi- o level-a-level, halafu chuo. Imani na mazingira ya kiuchumi tuliyojengewa ni magumu kiasi kwamba hatuoni njia nyingine za kumsaidia mtu apate ujuzi. 
-Usiwe kama yule tembo aliyefanywa kujiona ni dhaifu. Hao waliokufanya ujione dhaifu ni kwakuwa wanajua una nguvu na uwezo mkubwa wa kufikiri na kuwa bora zaidi. Amua leo kuwa mtu bora. Itachukua muda na ni ngumu, ila kuna thamani zaidi katika kujiona wa thamani.

Cheki video hapa chini ya jinsi Tembo anavyofanywa kuwa mtiifu. ONYO: Video inasikitisha


Share:

1 comment: