JE UMEFUMBIA MACHO JAMBO HILI LA KIMAENDELEO ?


Hakuna kanuni moja au muda muafaka wa kujua lini utafanikiwa hivyo usikate tamaa katika jambo la msingi unalofanya kwani pengine utakapokata tamaa utajikuta kumbe ungevumilia kidogo tuu mafanikio yangekuja.
Kumbuka hata waliofanikiwa sio kwamba kwao ilikuwa rahisi.
Watu wengi wanapofikiria mafanikio wanayatamani kwa kuyaona mazuri ila wanafumbia macho ukweli kuwa kuna kazi ya ziada katika kufanikiwa.

Kuna ugumu na kusota hata kama una akili za "ujiniasi" au kama kwenu ni matajiri, kama unataka kufanya jambo la msingi la maana maishani lazima utakumbana na ugumu fulani. Ugumu unatofautiana, sio lazima iwe ugumu wa kifedha, inawezekana kiutendaji, inawezekana ni kufikiria na kubuni bidhaa mpya, inawezekana ugumu wa kuongoza watu wengine, inawezekana hata ugumu wa kuelewa shughuli husika ili iwe bora zaidi.
Hata bosi wa Apple Steve Jobs hapo kabla aliwahi kufukuzwa katika kampuni aliyoianzisha kwa kuwa haikuenda vizuri. Leo hii watu wanatesa na Ipad -ujue kuna walioumia kuleta hivyo vitu.

--Amka sasa, magumu na changamoto zisikukatishe tamaa. Jua hiyo ni sehemu ya safari ya mafanikio. Kwa kuwa kuna magumu mengi katika safari ya kuwa wa kipekee na bora zaidi ndio maana wapo wachache wenye utofauti na maisha ya mafanikio. Je, hautaki kuwa mmoja wao ?

--Usiwe mtu wa kutoa visingio kuhusu UGUMU wako wa maisha au changamoto zako ziwe kisingizio cha kutopiga hatua. Kila mmoja ana changamoto. Fikiria jinsi ya kuzishinda badala ya kukubali kuwa ndio basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment