Biashara nyingi zilizopiga hatua kubwa ukizifuatilia zinaongozwa kiufanisi au tuseme "kisomi". Nchi nyingi zilizoendelea ukifuatilia namna wanavyoendesha nchi zao , ustaarabu na ufanyaji kazi ni wa kiwango cha juu kulinganisha na nchi yetu Tanzania.
Hata hivyo si ajabu kumsikia mtu nchini mwetu ukipendekeza mfanye jambo kiufanisi zaidi atakuambia aah hayo mambo ya kizungu, kibongo bongo haiwezekani.
-Nilishtuka kusikia wafanyabiashara kadhaa baadhi wana elimu za chuo kikuu, wengine hawana ila wote wana ndoto ya kufikisha biashara zao kwa viwango vya kimataifa wakisema eti mbinu za kisayansi na kiungozi ambazo tunasoma vitabuni na kwenye mtandao au kushuhudia wenzetu nje wamezitumia , ni kwamba hizo mbinu ni za kufikirika tuu.
Mbinu kama Mipango Mkakati (Strategic Plan) n.k. Watu hao wakiandaa vitu kama hivyo business plan , strategic plan n.k ni kwa ajili tuu ya kuonyesha kwa benki au wadau wengine lakini hawavitumii.
Watu hao wanabeza hata maneno ya kuhamasisha -Inspirational quotes wakisema hayo ni "maneno"tuu yasiyowezekana.
--Jiulize kwa akili nyepesi tuu, kama tunakataa kufuata mbinu bora za kujiletea maendeleo tukiendelea kujiambia kuwa kibongo bongo haiwezekani, je ni kweli tunawaza kwa usahihi mafanikio ya kufika mbali ? Kama tunataka kubadilika na kuwa bora lakini tuna mtazamo wa kufanya yale yale kwa mtindo ule ule, je mabadiliko tunayotamani yatakuja lini.
Hapa sizungumzii viongozi wa serikali , wao wana jukumu lao ila je wewe na mimi mienendo yetu ipo kimaendeleo?
0 comments:
Post a Comment