Fans, tafakari yetu ya ijumaa ya leo ni kuhusu utofauti wa maneno haya:
1. Nyepesi vs Rahisi
Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakianzisha jambo au kutamani kuwa kama wengine kwa sababu wanadhani kuwa hivyo ni RAHISI. Hata hivyo wanachoangalia wao ni WEPESI wa kufanya mambo fulani fulani. Nionavyo mie kitu kinaweza kuwa CHEPESI lakini kisiwe RAHISI.
Yaani UWEPESI upo katika uwazi na uwezekano wa yeyote kufanya jambo fulani, kwakuwa taratibu , na rasilimali zinawezekana kupatikana kwa yeyote anayetaka kufanya hivyo.
Mfano kuna wepesi kwa wengi kuingia katika kucheza MOVIES au kuanzisha blogs, lakini si rahisi kufanya fani hizo kwa mafanikio.
Urahisi ni swala linalotegemea uzoefu, elimu, ujuzi na bidii ya muda mrefu. Mfano kwangu mie kuandika posts kila siku ni kitu rahisi kwa kuwa tayari nina uzoefu na nina penda jambo hili. Kwa anayeanza kujifunza na asiyependa kuandika kwake ataona kuna WEPESI wa kupost ila akianza kazi hii ataona kumbe sio RAHISI.
2. Kuwa na ulemavu vs Kukosa uwezo: Kwa kiingereza tunasema DISABILITY is not INABILITY.
Yaani mtu anaweza kuwa na ulemavu ambao unaweza kweli kuchukuliwa na wengi kama ndio kutokuwa na uwezo wa kufanya jambo fulani au kujiwezesha kiuchumi.
Hata hivyo wapo wasio na miguu na wanacheza basketball, wapo wasio na mikono miguu ila ni matajiri.
La msingi ni kumbuka kuwa vile unavyoweza kuwa sio matokeo ya mazingira yako bali ni namna wewe unavyochukulia na kutumia mazingira yako kufanya kweli.
3. Ngumu vs Kutokuwezekana
Mara nyingi wengi wamekata tamaa pale mambo yanapokuwa magumu, wakijiambia kuwa haiwezekani. Kinachowatofautisha watu makini, watu maliofanya mambo makubwa sio kwamba katika shughuli zao hawakukumbana na magumu, bali walijizatiti na kukabiliana nayo. Bahati zipo ila wewe kwanza inabidi usimame imara, ukabiliane na magumu -usione magumu kama ndio alama ya kushindwa.
Nikuache kwa msemo huu toka kwa Allan Rufus, katika kitabu chake The Master's Sacred Knowledge :
“Hard work does not go unnoticed,and someday the rewards will follow”-- "Bidii ya kazi haitokaa ipotee bila kutambulika. na ipo siku malipo yatakuja."
0 comments:
Post a Comment