Kwa huduma kama Google Drive, Dropbox, unaweza kujikuta hauhitaji kuwa na flash disk. |
Lengo
basi la Makala hii ni kukupa dokezo la njia mbadala ya kutunza files na folders
ambapo, files na folders zako zitakuwa zipo ‘hewani’- mtandaoni hivyo hautokuwa
na hofu ya kupoteza kazi zako kwa njia tulizotaja hapo juu.
Ili
kuhifadhi mtandaoni files na folders zako, unaweza tumia huduma mbalimbali kama
vile:
Google Drive, Box
, CloudMe , Dropbox , Droplr , iCloud , Mega
, SkyDrive , SparkleShare
, SugarSync , Ubuntu One
na Yandex
Disk.
Katika
makala hii tunachambua kwa ufupi huduma za Google Drive, Box, na Dropbox. Sehemu yetu ya kwanza leo hii tunatazama Google Drive.
Kuanza kuitumia Google Drive
Ili
kutumia huduma hii, inakupasa uwe na akaunti ya Gmail. Kisha ingia kwa website
ya Google Drive,
andikisha akaunti yako ya Google Drive. Google wanakupatia 5GB za bure
ili uweze kuhifadhi mambo yako humo Google Drive. Ukitaka kuongeza
ukubwa wa Drive, basi itakubidi ulipie kwa kufuata maelekezo ya jinsi ya
kuongeza ukubwa wa Google Drive.
Jinsi ya kuhifadhi files na folders kwa
Google Drive
Unapotaka
kuhifadhi files au folders inabidi uingie kwenye website hiyo ya Google Drive,
halafu nenda sehemu ya Upload. Angalia picha hapa chini. Hii inamaanisha kuwa
unaweza kupata files na folders zako popote pale utakapokuwepo. Ni kama vile
kuwa na flash disk, isipokuwa kwa Google Drive inabidi uwe umeunganishwa na
mtandao (internet).
Kuinstall Google Drive kwa Kompyuta yako
Huduma
ya Google Drive, inakuwezesha pia kudownload program ya Google Drive, hivyo
ukiwa ume install hiyo program kwa kompyuta yeyote utaweza kuwa unatupia tuu
files na folders zako kwa kompyuta, kisha utaweza kuziona popote pale
utakapoenda mtandaoni.
Hata
hivyo kumbuka, sio lazima ku install Google Drive kwa kompyuta. Unatakiwa
kufanya installation endapo tuu unataka kuwa na uwezo wa ku dumbukiza mafaili
yako kwa kutumia kompyuta. Na pia kama unataka kuwa unafungua faili lililopo
katika Folder lako la Google Drive, na ku save humo, basi moja kwa moja
mabadiliko uliyoyafanya katika faili hilo yanakuwa yamefanyika katika Google
Drive iliyopo hewani (mtandaoni).
Itumie Google Drive kwa Kuandaa kazi
mbalimbali
Unaweza
pia ukatumia Google Drive kuandika kazi zako mbalimbali, kama vile ufanyavyo
kwa kompyuta binafsi kwani Google Drive ina program ya WORD, POWEPOINT na EXCEL.
Ukishaandika kazi zako unaweza ukazihifadhi humo humo Google Drive, au ukaamua
kuzituma sehemu yeyote uitakayo.
Unaweza Kushare files
na folders zako zilizopo ndani ya Google Drive
Matumizi mengine ya msingi ya Google Drive ni kukuwezesha
kutuma files na folders ambazo ni kubwa sana kiasi haziwezi kutumwa kwa kutumia
njia ya email. Unachotakiwa kufanya weka files au folder lako kwa Google Drive,
kisha nenda sehemu ya Share kulia mwa Google Drive, halafu fuata maelekezo ya
jinsi ya kushare file au folder husika.
Kwa sababu inakupa uwezo wa kushare files na folders na watu
wengine, Google Drive inakupa nafasi ya kufanya kazi kwa kushirikiana na watu
mbalimbali. Kwani waweza andika kazi, uka isave kwa Google Drive, mtu mwingine
akaja aka edit, au kuongeza kitu, kisha nae akasevu humo.
matumizi ya hii google drive yanatumika kwa computer pekee hayawezi tumika kwa simu za android ?
ReplyDeleteJifunze kuandaa blog.. website ..card mbalimbali..ema em..matangazo online.gogo adsense..tunafundisha online polite ulipo...kà ribu ulimwengu wa digital ..pigaa 0764839091
ReplyDelete