MAMBO YAKUFANYA KIPINDI HIKI CHA COVID-19 KAMA WEWE NI MJASIRIAMALI


coronavirus covid-19 na wajasiriamali

Tishio la ugonjwa wa virusi vya Corona  (COVID-19) ni kubwa sana. Tayari shirika la afya duniani (WHO) limetangaza kuwa COVID-19 ni janga la dunia. Athari za COVID-19 kwa biashara ni kubwa sana ikiwa ni pamoja na biashara nyingi kufungwa, wafanyakazi kupoteza ajira, wengine kupunguziwa mishahara na hata baadhi ya biashara kuanza kutangaza kufirisika. Katika makala hii tunakuelezea ni mambo gani unayoweza kufanya kama unamiliki biashara ili uweze kupita salama katika kipindi hiki kigumu.
Chukua tahadhari za kiafya zinazoshauriwa:
Uhai una thamani kubwa sana kuliko faida au biashara unayoihangaikia. Hivyo usihatarishe maisha yako kisa kutaka faida. Hapa tunamaanisha nawe mjasiriamali chukua tahadhari zote zinazoelekezwa katika kujilinda dhidi ya Coronavirus ikiwemo kuosha mikono  kwa maji yanayotiririka, kutopeana mikono na watu, kukaa mbali na watu wenye dalili za kuwa na COVID-19 na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Jenga brand yako:
Huu ndio wakati ambapo watu wengi watatumia mtandao iwe ni kwa simu au kwa kompyuta, hivyo ni wakati mzuri sana kwako mjasiriamali kuweka machapisho sio tuu yanayotangaza bidhaa au huduma yako bali yanayoweza kujenga brand yako, yaani machapisho yatakayoonyesha wewe ni mtu wa aina gani, biashara yako inaamini katika nini, na uguse hisia za watu kwa namna ya kipekee.
    
Jiandae kupunguza bei za bidhaa au huduma zako:
Huu ni wakati ambapo watu wengi hawatokua na kipato cha kutosha kufanya manunuzi kama walivyozoea. Wengine watakua wamekatwa mishahara, na wengine vyanzo vyao vya mapato vitakua vimekauka. Hivyo kupunguza bei ni namna ya kuwafanya wateja wako waweze kweli kufanya manunuzi.
Weka mipango ya kupunguza gharama za uendeshaji na malipo mengine mapema kabisa:
Kwakua hautopata mapato kama kipindi  kabla ya janga la Coronavirus , inakupasa ujipange sasa namna ya kupunguza gharama zako ili kwamba usishindwe kuzifanyia malipo. Njia za kupunguza gharama za uendeshaji zinaweza kuwa: Kufanyia kazi majumbani , kuacha matumizi ambayo sio ya lazima, kupunguza wafanyakazi, kupunguza mishahara, kuomba kuahirisha kufanya malipo fulani kama vile kuomba ulipe madeni baada ya miezi mitatu toka sasa n.k.
Weka mipango ya namna ya kukopa kwa unafuu
Kwakua kuna uwezekano utakosa mapato ya kutosha kutokana na hali ya kiuchumi kuwa ngumu , basi utakuja kuhitaji fedha za kuendesha biashara yako au hata kulipia marejesho ya mikopo yako ya zamani. Ni wakati sasa wa kuanza kufuatilia wapi unaweza pata fedha ya mkopo. Sio lazima ukope benki, waweza angalia vyanzo vingine kama vile watu binafsi au asasi nyingine zenye kutoa misaada kwa wajasiriamali.
Hitimisho:
Tuwasiliane kama unahitaji ushauri au namna ya kuwafikia wateja ili kuendelea kuboresha biashara yako. Tumia namba +255 623 029 683 tuwasiliane kwa WhatsApp au kwa namba ya kawaida.

Share:

0 comments:

Post a Comment