JINSI YA KUINGIZA BIASHARA YAKO MTANDAONI



kufanya biashara mtandaoni

Katika ulimwengu wa kidigitali tulionao biashara yako inahitaji kuwa mtandaoni (online), lakini katika nyakati hizi za tishio la ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19) sio tena swala la hiari kuwa mtandaoni bali kuwa mtandaoni kunageuka kuwa ni lazima kama unataka kuendelea bado kufanya biashara. Hii ni kwa sababu ya hali ya wasiwasi wa maumbukizo na marufuku ya kuwepo kwenye mikusanyiko ya watu wengi.
Fanya mambo yafuatayo ili nawe ufanye biashara kupitia mtandaoni:
1.Uwe na Website:
Unahitaji kuwa na sehemu moja mtandaoni ambapo watu watapata taarifa zote za msingi kuhusu biashara yako kwa namna ambapo zitakua zimepangiliwa vema. Sehemu hiyo ni website. Utakua na anuani ya website yako ambapo watu watapata kuingia kwa kupitia browsers kama vile Google Chrome, Internet Explorer , Mozilla Firefox n.k.  Unahitaji website hata kama unazo akaunti za social media kwakua website itatoa maelezo yote kuhusu website yako kwa namna bora zaidi kwani utapangilia taarifa zako vema, na pia ni sehemu rahisi ya kuanza kujenga uwezo wa watu kuifikia biashara yako hata wakiwa wanasearch mtandaoni.
2. Anza kuandika Blog:
Unahitaji kuandika mara kwa mara machapisho yatakayojibu changamoto na kuwapa wateja watarajiwa taarifa za msingi wanazohitaji. Hii itawafanya watu wawe karibu na biashara yako , waifahamu vema na bidhaa zako na mwisho wa siku watake kufanya biashara nawe.
Mfano unauza nguo, unaweza kuwa na blog inayozungumzia mavazi, fashion na namna ya kuwa na muonekano bora na mvuto. Watu watakaosoma blog yako watapendezwa na kujitoa kwako kuwasaidia na pia watajifunza kuhusu biashara yako inavyoweza kuwapatia mavazi na vitu vingine ili waweze kuwa vile ambavyo wewe umeelezea kuwa wanahitaji kuwa ili wawe na muonekano bora na wenye mvuto.
3. Wekeza kwenye kutumia Social Media kwa ubora zaidi
Haitoshi tuu kupost kuhusu bidhaa au huduma zako ukiwataka watu wanunue. Unahitaji kuwa ‘social’ yaani ujichanganye na jamii kwa kuwa na vitu tofauti tofauti vya kupost zaidi ya bidhaa. Utumie social media kama Facebook, Instagram, Twitter na WhatsApp kujenga brand yako ili uweze kuwa na uwezo haswa wa kushawishi watu kuhusu bidhaa au huduma zako. Pia social media ikusaidie kuwafanya watu watembelee website pamoja na blog yako.
Unaweza kuwa na magroup ya WhatsApp na Facebook ili uweze kuendelea kuwa karibu na wateja wako, ukiwaelimisha na kuwasaidia kujenga mtandao kati yao ili mwisho wa siku ujenge jamii (community) inayojumuika pamoja kupitia brand yako.

4. Lipia matangazo ya mtandaoni
Kulipia matangazo kama vile ya Facebook, Instagram , Google Ads na mengineyo ni muhimu sana haswa kwa ajili ya kupata watu wengi zaidi waone kile unachokitangaza kwa haraka. Hata hivyo usibweteke na matangazo hayo kuwa yatavuta watu na kujenga brand. Inakupasa uendelee kuwekeza kwenye kuelimisha, kuburudisha na kuwashirikisha watu wakuelewe kwa ukaribu zaidi na waipende biashara yako.

Hitimisho:
Umuhimu wa kufanya biashara mtandaoni una umuhimu mkubwa sana katika kipindi hiki, lakini ili ufaidike na mtandao unahitaji kujipanga vema katika kuingia mtandaoni. Sasa umeshajua mambo hayo makuu matatu ya kufanya ili uingie mtandaoni. Jibidiishe ufanye vema. Mtandao unalipa. Ukiwa na swali au unahitaji  tukusaidie kutekeleza na kusimamia mpango huo wa kuingia mtandaoni, tafadhali tuwasiliane kwa namba +255 623 029 683 kwa simu ya kawaida au kwa WhatsApp kwa namba hiyo hiyo.

Share:

0 comments:

Post a Comment