JINSI YA KUWA NA BLOG YA KULETA WATEJA WA BIDHAA AU HUDUMA YAKO

Hakuna biashara bila kuwa na wateja, na Hakuna mauzo kama wateja unaotarajia hawanunui bidhaa zako. Kama unajiuliza utafanyaje ili upate mauzo ya kutosha mtandaoni basi endelea kusoma hapa maana utagundua kanuni na mbinu ambazo zitakuwezesha kuongeza mauzo  ya bidhaa zako haswa kama unataka kufanya mauzo mtandaoni.
Usikose darasa maalum kuhusu blogs na biashara kwa undani zaidi na mada nyingine, ni jumapili hii Julai 16, kuanzia saa tatu usiku kupitia WhatsApp na FB. Tuwasiliane upate utaratibu wa kujiunga na darasa hilo..

Mtazamo sahihi kuhusu kuuza
Jiulize je mtu anaweza nunua basi kwa ajili ya kufanya biashara ya Dar hadi Zanzibar ? Au kununua meli kwa ajili ya kusafirisha mizigo kati ya Iringa na Mbeya? Bilas haka jibu ni hapana, hivyo hivyo mtu hawezi kukutafuta kwa bidhaa au huduma yako kama bidhaa au huduma yako haikidhi hitaji lake.
Kazi yako kuwa katika blog yako ni kuonyesha bidhaa au huduma yako inaweza kweli kukidhi mahitaji yake.

Jinsi ya kutangaza vema bidhaa au huduma zako kupitia blog yako mwenyewe
Kuna namna mbili ya kuelezea bidhaa zako kwa mteja. Moja ni njia ya moja kwa moja , na nyingini ni njia isiyo ya moja kwa moja ila mteja mlengwa ataweza kuunganisha ‘picha’ na kujua nini haswa unauza na kuelewa namna gani na  yeye anaweza kunufaika na huduma au bidhaa zako.
Njia ya moja kwa moja ya kutambulisha bidhaa na huduma zako kupitia blog yako
Hii ina maana ya kuelezea wazi wazi kupitia matangazo yako katika blog. Zaidi ya matangazo unaweza weka ukurasa maalum wa PRODUCTS au SERVICES halafu katika ukurasa huo ukaelezea hizo bidhaa zako.
Wengine hutumia pia ukurasa wa CONTACT US kuelezea kile wanachouza.
La msingi la kukumbuka ni kuwa watu hawaji kwa blog yako kusoma kuhusu bidhaa au huduma zako hivyo hakikisha haujazi blog yako kwa matangazo , au habari ya nini unauza.

Njia isiyo ya moja kwa moja ya kutambulisha bidhaa na huduma zako kupitia blog yako
Mfano mzuri wewe usomapo ujumbe huu tayari unaweza kupata picha aina gani ya huduma sisi tunatoa, nap engine bila hata kukuambia wewe mwenyewe unaweza kutaka kututafuta tukusaidie kuhusu blog yako au kuhusu mbinu za ujasiriamali na masoko. Kama umeliona hilo haujakosea kabisa, ndivyo ambavyo hata wewe ukiwa na blog na kuandika kwa umakini utaweza kueleza vema kuhusu bidhaa au huduma zako.
Njia isiyo ya moja kwa  moja ya kuelezea bidhaa na huduma zako kwa mteja, inahusika na wewe kama wewe kujionyesha kweli unajali yale wateja wako wanayopitia, hivyo unawaelezea nini kinaweza kuwatoa huko walipo. Kwakufanya hivyo utakua unatangaza huduma au bidhaa zako kwani bidhaa au huduma zako zinaweza kuondoa hayo ambayo watu wanakumbana nayo.
Sisi Mbuke Times mara zote hufanya hivyo na tunaona matokeo makubwa sana.
Mfano mzuri  ni vile ambavyo tumekua tukipokea wanafunzi wa kuwafundisha English kwakua wamesoma mbinu na miongozo mingi kuhusu English kutoka kwa blog yetu.

Weka wateja wako mbele kwanza
Fikiria yale wanayohitaji kufahamu na uandike kuhusu hayo kwa kuhusanisha na kile ambacho wewe unauza.
Fanya iwe rahisi watu kusoma blog yako, tumia vizuri rangi za background na rangi za maandishi. Tumia picha na vielelezo vingine Zaidi ili kweli unachoandika mtu akielewe.
Tumia muda kufanya utafiti wa unachoandika na pia utumie muda wa kutosha kutafakari na kupangilia mawazo yako ili unachoandika kivutie na kieleweke vema.
Wateja wako wataona jinsi unavyowajali kwakua muonekano wa blog yako na kile  unachoandika kitakuelezea wewe ni mtu wa aina gani haswa.

Namna ya wasomaji kuwasiliana nawe
Hakikisha blog yako imetaja wazi njia zipi ambazo wateja wako watarajiwa wanaweza

Jiandae kuuza kwa wale watakaotembelea blog yako
Blog sio sokoni kusema watu waje wanunue bidhaa au huduma zako. Blog ni mahali ambapo unatakiwa kuwafanya wale ambao sio wateja, wafikirie kuwa wateja. Itahitaji watu hao wasome Makala zako nyingi sana ili waweze kweli kujiridhisha na bidhaa au huduma zako, usijali hilo.
Kumbuka wapo watu wanaokuja kwa blog yako kwakua tuu walikuwa wanatafuta taarifa Fulani Fulani, hao sio kwamba wapo tayari kununua. Wanaweza kusoma blog yako na kuhifadhi jina la blog yako kwa ajili ya baadae watakapokuhitaji.
Kuna ambao watakuja kwa blog yako kwakua wapo tayari kununua. Hivyo ukikoleza maelezo yako vema na kuonyesha kweli wewe unaweza kuaminika , watu hao wanaweza kuja kukutafuta.
Kumbuka katika hali zote, mtu akikutafuta sio kwamba ndio tiketi kwako kuwa tayari mauzo yamekamilika. Unahitaji bado kuendelea kumuonyesha kwanini akuamini na kununua toka kwako.
Inakupasa uwe na lugha nzuri, uweze kutumia KANUNI ZOTE ZA MSINGI ZA KUFANYA MAUZO.

Call to Action zinahitajika katika blog
Je blog yako na Makala zako zina call to action? - yaani kile ambacho unataka watu wafanye kabla ya kuondoka hapo kwa blog yako ? Calls to actions inabidi ziwe na lugha nzuri na zijikite kwa mteja na kile anachoweza kupata toka kwako.

Fanya utafiti
Ni kweli kuwa watu wengi huandika blog kama hobby au kitu wakipendacho. Hata hivyo kumbuka hobby yako au ukipendacho sio  lazima kiwe ambacho watu wanahitaji au kinachoweza kukuingizia mapato ya kutosha.
Fanya utafiti kuhusu jamii na haswa wasomaji wako na fans wako kwenye mitandao ya kijamii. Utapata kujua nini haswa kinahitajika.

Sikiliza wasomaji wa blog yako
Soma comments, messages na emails toka kwa wasomaji wako. Utaweza kugundua nini haswa wanahitaji wewe uwaambie , na nini cha kuboresha. Hii pia itakufanya ujue namna gani bora Zaidi ya kutambulisha bidhaa na huduma zako kwao.
Mfano mzuri hata post hii unayosoma ni kwa sababu ya swali la mmoja wa wasomaji wangu aliyetaka kujua atafanyaje awe na blog inayomuingizia hela kupitia huduma zake kama mtaalamu wa mambo ya saikolojia. Mie nimeamua kuongeza zaidi ili jibu langu liwanufaishe watu wengi zaidi.

Umakini na ubora wa unachopost katika blog yako
Kazi kubwa ya blog katika kufanikisha mauzo ya bidhaa au huduma yako ni kujenga uelewa kuhusu nini unauza , kujenga uelewa wa wewe ni mtu wa namna gani, na Zaidi sana kujenga kuamini na kutegemewa na wale wanaosoma Makala zako.
Hivyo wekeza kweli kweli katika kile unachoandika kiasi kwamba atakayesoma apate picha ya juhudi na kazi uliyonayo katika kuwafikishia ujumbe na hivyo watu hao watategemea.
Kwahiyo ingawaje unahitajika kuandika Makala mara kwa mara, haina maana basi ndio ‘ulipue lipue’ ili mradi tuu uwe na Makala. Wasomaji wako wanajua kutambua Makala zilizoandikwa kwa umakini na kwa kujitoa kweli kweli, na zile Makala zilizoandikwa ili mradi tuu kutaka watu watembelee blog yako.
Ukiandika Makala kwa umakini na upendo mkubwa watu watataka pia kushare na hata wenye blog wengine watataka waweke kwa blog zao na kutaja wewe na blog yako hivyo kujijengea kufahamika Zaidi.

Search Engine Optimization
Unahitaji kuandika kwa umakini lakini pia kuandika kiasi kwamba search engines kama vile Google, Bing na Yahoo waweze kuzifikia Makala zako kwa urahisi na kuorodhesha Makala zako katika ukurasa wa mwanzo pale mtu anaposearch mtandaoni.
Search Engine Optimization inakuhitaji uangalie namna utumiavyo maneno yanayoweza kutafutwa mara kwa mara , pia ujue namna ya kuandika vichwa vya habari, picha zenye majina sahihi na maelezo mengine sahihi, pia Makala iwe na wingi unaofaa wa maneno sio tuu ka Makala kafupi ka aya moja.


Share:

3 comments:

  1. Nahitaji kuwa na blog nifanyeje jamanii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fuatisha maelekezo yaliyopo katika makala hii na makala nyingine kuhusu kuwa na blog ambazo unaweza kuzisoma kwa kubofya link hii https://mbuke.blogspot.com.co/search?q=blog
      Ukihitaji msaada zaidi wasiliana nasi kwa WhatsApp namba +57 301 297 1724.

      Delete
  2. Mimi na blog ila jaiunganisha na yahoo na Google wala mtandao wowote wa kijamii nifanyaje jamni nsaidien

    ReplyDelete