UNAFAHAMU HILI KUHUSU HATERS WAKO (WANAOKUCHUKIA) ?

Tafakari yetu leo inahusu HATERS (Wale unaoamini wanakuchukia).
Unaamini kuna watu wanakuchukia kwakuwa unadhani wanakutakia mabaya, unaamini hawakupendi na wanamipango ya kukurudisha nyuma. Hawapendi furaha yako, na wanasubiria tuu uanguke. Unawachukie na pengine umeshaandika status maalum juu yao hapa FB, au upo njiani zikikupanda siku unawapa “makavu” live kwa kuchafua wall yako.
Ndio, unastahili kuwakasirikia, unastahili kutokufurahia wayafanyayo na unastahili kujipanga ili haters wasifanikiwe wanachofikiria juu yako. Ila leo nataka kukukumbusha hater mmoja aliyejificha na anayeweza kukumaliza kwa uharaka kwa kuwa pengine haujamshtukia. Hater huyo ni wewe mwenyewe kwakuwa:-
Kuna mambo ya msingi unatakiwa uyafanye ila umekuwa mtu wa kutafuta visingizio usikamilishe hayo mambo ya msingi. Kwa mtindo huu unafanana na haters kwani unajikosesha fursa wewe mwenyewe. Acha visingizio , jitume kweli kwa hicho ulicho nacho, kwa mazingira uliyo nayo.
Wewe pengine umekuwa ukiwafanyia wengine ubaya au visa, pengine si kwa chuki ila unafanya hivyo ukiamini ni haki yako ili ufanikiwe. Matokeo yake ni kuwa unajijengea chuki na uadui kwa wengine. Unajikosesha uaminifu hivyo kujiharibia wewe mwenyewe kama hao haters wanavyotamani kukuharibia.
Hauamini katika uwajibikaji ili kusaidia jamii. Unadhani la msingi ni bora wewe upate , mkono uende kinywani. Hata hivyo kwa utendaji wako mbovu, kwa kutokuwajibika kwako iwe kielimu , kibiashara , kimalezi n.k jamii yetu inaporomoka siku hadi siku. Haulioni hili kama ni janga litakalokuja kuumiza wewe mwenyewe pia. Na cha ajabu upo makini kulaumu wengine kuhusu maisha magumu na mporomoko wa maadili na hali ya kiuchumi.

Ok, wakati unaweka mikakati ya kupambana na haters, weka pia mkakati wa kuwa mtu bora zaidi kila siku, ili upunguze madhara unayojijengea siku hadi siku kwa maisha yako mwenyewe.
Nikuache na msemo huu toka kwa  William Faulkner:
“Unless you're ashamed of yourself now and then, you're not honest” 
" Isipokuwa tuu unajisikia nyakati fulani fulani aibu kuhusu wewe mwenyewe, jua haupo mkweli".
Share:

0 comments:

Post a Comment