SASA WAWEZA UNGANISHA FRIJI NA INTERNET: FAHAMU NINI MAANA YA INTERNET OF THINGS

Kuwa kuna kitu kinachoenda kubadili maisha yetu ulimwengu wa namna ya ajabu. Kitu hicho kinaitwa Internet ya Vitu (kwa kizungu : Internet of Things). Ipo hivi:-
Fikiria upo mezani unatumia kompyuta yako, mara kengele ya saa ya mezani inalia kukuashiria kuwa umefika muda ujiandae kwa ajili ya mkutano, wakati umenyanyuka toka kitini tayari mlango umejifungua, na tayari bafu limekwisha cheki kuhakikisha maji yapo tayari kwa ajili ya kuoga. 
Wakati huo gari lako limeshapokea taarifa ya barabarani tayari kukuambia njia gani hazitokuwa na foleni. 
Wakati unataka kutoka friji linakupa taarifa kuwa nyama uliyoweka humo kwa muda wa wiki nzima sasa haifai kuliwa, na kwamba mayai yamepungua unahitaji kuweka oda mpya.
 Unapotoka ndani kwenda kwenye gari wala hauhitaji kujiuliza kuwa gari lina mafuta au la, kwakuwa tayari ulishapokea taarifa ya gari lako kama lina mafuta , kama matairi yote yana upepo n.k.

Hapo juu ni mfano wa Internet Of Things (IoT). Ipo hivi, kwa sasa internet tunayotumia wengi wetu ni ile ambayo inatutaka sisi binadamu kufanya kazi ya kufikisha taarifa kwa computer na kompyuta yenyewe inafanya kusambaza kwa kompyuta nyingine ili watu wengine wazione na kuzitumia hizo taarifa. 
Mfano mie nimekaa kwa kompyuta yangu na kuandika Makala hii, kisha kupitia kompyuta au simu yako wewe umeipata.  
Hata hivyo kuna Zaidi ya Internet ya namna hii , ambapo vitu vyenyewe kwa vyenyewe vitawasiliana na kupeana taarifa, kuzitumia bila wewe binadamu kuhusika. Ila wewe waweza kuona taarifa husika na kuzitumia kufanya mambo kadha wa kadha.
Mfano niliokupa hapo mwanzo ni kuwa gari kwa mfano lenyewe linawasiliana na vifaa vingine vinavyoratibu foleni za barabarani hivyo kupata taarifa, taarifa hizo zinahifadhiwa pengine taarifa hizo zinaweza kutumwa kwa kifaa chako kinachoratibu ratiba zako za mikutano, ili kukurekebisha taarifa za safari zako. Friji linawasiliana na vitu vilivyopo ndani mfano chupa za bia au soda ili kujua kama soda ni za baridi au moto, kama zipo idadi ya kutosha au la. 
Friji lenyewe linaweza kuagiza soda zaidi endapo zilizobaki ni chache.
Wataalamu wa teknolojia ya mitandao na vifaa vya kielektroniki wanatumia teknolojia ya sense na kuweka anuani maalum kwa vifaa husika, pia spidi ya internet iwe bora na ya uhakika.

Angalia video hii hapa chini kuelewa zaidi swala hili la Internet of Things.

Share:

0 comments:

Post a Comment