TAFAKARI YETU YA LEO: JINSI YA KUWA MWENYE FURAHA

Ukitafakari kwa umakini na kujiuliza vema utakuja kugundua kuwa majibu ya maswali yafuatayo yote yanaangukia katika JIBU moja kuu –  NI KWAKUWA  UNATAKA KUWA MWENYE FURAHA.
Maswali yenyewe ni:-
Kwa nini unatamani kuwa na mpenzi , mume au mke mzuri na mwema
Kwa nini unatamani kuwa na kazi nzuri au biashara yenye mafanikio
Kwa nini unataka watoto , tena watoto hao wakue vema, wakuheshimu na wafanikiwe
Kwa nini unahitaji mtandao mzito wa watu wengi wenye manufaa kwako
Kwa nini unachukia ‘haters’ wako
Na maswali mengine kama hayo, waweza ongeza hapo chini kwenye comments.
Kumbe Furaha ni muhimu kiasi hicho , hata hivyo unaweza kuwa unakosea sana kama umejiweke fikra kuwa FURAHA ni kama kitu unachokipata ukifika KITUO FULANI. Yaani furaha yako ni pale utakapo pata kazi bomba, furaha yako ni pale utakapowakomesha maadui, utakuwa na furaha pale utakapo piga hela ndefu katika biashara, utakapompata mpenzi , mke au mume wa ndoto yako, n.k. Kwa fikra ya namna hiyo waweza jikuta haufurahii maisha, unajikuta kila wakati una deni la kutimiza kitu fulani ili eti ufurahie maisha.
Elewa Furaha ni swala la fikra zaidi kuliko mazingira, watu au vitu vinavyokuzunguka.  Jifunze kujitambua, anza kwanza kuthamini uwepo wako tuu kama kiumbe hai. Uhai wako ni sehemu ya furaha tosha.
Furaha yako iwe ni kwa kila unachoweza kukifanya kiwe kikubwa au kidogo. Furahia kuwa unathamini maisha na kwamba furaha yako inatimia pale kila siku unapoweza kuongeza kitu hata kama ni kidogo katika maisha yako.
 Jiamini, jua una deni kubwa la wewe mwenyewe kujisikia vema kuhusu uwepo wako. Kisha anza kufanya kweli mambo ya msingi. Usiogope mazingira uliyo nayo, usiogope nini kitatokea ukikosea, wewe kuwa makini vya kutosha na jitoe kweli katika kila ufanyacho.

Karibu kila mtu ana mazingira ambayo anatamani yangebadilika, hata hao matajiri nao wana matatizo yao , hata hao wenye waume na wake ‘bomba’ nao pia wana changamoto zao, hata wenye biashara kubwa nao wana magumu yao. La msingi katika furaha sio WEPESI gani unao kimaisha bali ni kwa namna gani fikra zako zinashinda changamoto ulizo nazo. Usifikirie FURAHA kama kitu utakachokipata ukifika kiwango fulani cha maisha.
Share:

1 comment:

  1. Nimekuwa nikitaka kuwa wa ndugu mkubwa wa ILLUMINATI kama nilikuwa na hamu kubwa ya utajiri na umaarufu na kwa jitihada zangu nimeingia katika baadhi ya mikono isiyofaa kunidai kunisaidia kupata punguzo la uanachama na nimepata maradhi ya fedha yangu. Hivi karibuni nimepata ajira ya haki na wajumbe kwenye illuminatiworldofriches6666 @ gmail. com au +2349034745112

    ReplyDelete