KATIKA NCHI HIZI JINA LAKO NI LAZIMA LIKUBALIKE KISHERIA

KAMA HAUKUJUA BASI JUA
Kuna nchi duniani zimeweka sheria kabisa kuhusu namna ya kuwapa majina watoto wachanga na pia kudhibiti wale watu wazima wanaotaka kubadili majina yao.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa kuna watu huamua aina ya majina ambayo pengine yanaleta hisia mbaya katika jamii -mfano wapo wanaoamua kujiita jina ambalo linajulikana wazi ni TUSI.
Wapo ambao hutaka kutumia majina ambayo tayari yana maana maalum katika jamii mfano mtu anajiita MUNGU, MFALME, RAISI, au SHETANI.
Na kuna wale ambao huamua tuu kuleta usumbufu usio wa lazima kwa kujiita jina refu mfano Mdeyeldofyeoffeikyegoedyeedoedofdd.
-Yaani hata hauelewi ni kitu gani !
Kwa mujibu wa CNN, nchini New Zealand serikali imepiga marufuku kwa mtu kuwa na jina MASIAH, au Lucifer, Yesu,Haki,Mfalme. Kuna wazazi wao walijitokeza na kuwapa watoto majina ****, wengine """". Yote yalikataliwa.
Embu ona wengine walitaka majina haya: "Mafia No Fear." "4Real." 
Nchini SWEDEN kuna mzazi alitaka kutumia jina:
"Brfxxccxxmnpcccclllmmnprxvclmnckssqlbb11116."
Sijui hata unalitamkaje !
Jamhuri ya Dominika iliweka vizuizi vya majina baada ya wazazi kuanza kuita watoto majina ya magari na matunda. Hahaa.. kwa mtindo huo waweza kukuta mtoto anaitwa "BMW", mwingine "HIACE" au  "NANASI".
Kwa uhondo zaidi soma makala hizi mbili toka CNN:
1. Makala ya kwanza BOFYA HAPA
2. Makala ya pili . BOFYA HAPA
Share:

0 comments:

Post a Comment