JINSI YA KUOMBA MSAADA (MCHONGO) KWA UFANISI

MUHIMU KUJUA KUWA 
Unapoomba msaada kwa mtu kisha akakaa kimya inakupasa:
1. Uendelee kukumbushia: Kwakuwa wengine huwa bize kweli kweli kiasi kwamba kiukweli wanapitiwa. Kama mtu anasahau mambo ya msingi ya familia yake sembuse wewe mtu wa nje kukumbuka ulichoomba.

2. Fuatilia : Kwakuwa wengine huhitaji kuona ni kwa jinsi gani upo na uhitaji wa swala husika.

3: Unyesha juhudi binafsi ulizofanya kupata kitu husika na ukashindwa au sehemu gani haswa ya tatizo hilo ndio unahitaji msaada. Mara nyingi kama wewe mwenyewe tuu haujaonyesha kujituma katika kutatua tatizo husika, basi hata huyo unayemuomba msaada unakuwa umemkatisha tamaa. Yaani haumpi sababu ya kulichukulia jambo kwa uzito wa kipekee na kwa haraka.

4: Hata kama utaambiwa haiwezekani au mtu husika akashindwa kukusaidia usilifanye jambo hilo liharibu mahusiano yenu. Tunasema kwa kiingereza "Don't take it personal".  Na zaidi sana usijichukie na kujishusha thamani kwa kukosa msaada toka kwa mtu fulani. Usiamini haujasaidiwa kwa sababu fulani binafsi kuhusu wewe. Amini kwa kiwango kikubwa  wewe kama wewe hauna tatizo mpaka ukashindwa kusaidiwa, bali inawezekana: Ni huyo mtu mwingine namna anavyofikiria mambo, inawezekana pia ni kwa sababu ya vikwazo vya kuwasiliana vema au pengine jambo husika bado halijafikia wakati muafaka, hivyo wewe "komaa" kuboresha hicho ulichonacho ili kufanikisha kutatua tatizo lako.

5. Unapoambiwa hapana na mtu fulani, haimaanishi kuwa HAIWEZEKANI. Haimaanishi kuwa mtu huyo ndio KASHAFUNGA MILANGO yote. Kushindwa kwa mtu fulani kukusaidia badala ya kukutisha tamaa, iwe kinyume yaani kukupe hamasa ya kutafuta zaidi suluhisho la tatizo lako. 
Mfano mzuri ni wakati naanza kuandika blogs, pamoja na kupenda kuandaa blogs sikujua hata namna ya kuandikisha blog. Kuna watu niliwaomba wanisaidie wakawa wananipiga kalenda, wengine walikaa tuu kimya pamoja na kukumbushia mara kwa mara. Hata kuedit template ya blog ili iwe bora ilishindikana. Ikanibidi kujifunza vyote mwenyewe hadi sasa nimeweza hata kuandika kitabu cha HTML na CSS kuwasaidia wengine. 
Kitabu hicho kinakupa mwanga wa jinsi ya kuandika codes kwa kutumia HTML na CSS, na pia kukupa muongozo wa jinsi ya kubadili muonekano wa blog yako iwe bora zaidi kwa kutumia uelewa wako wa HTML na CSS. 
Kinapatikana kwa Tshs. elf6 tuu kwa lugha ya kiswahili. Wasiliana na Mushi Richard, (fb: Bwana Mushi), Mpesa: 0755872462, Tigopesa: 0713643703. Mtumie fedha atakutumia soft copy kwa email.
Share:

10 comments:

  1. Naitwa owden mwakisambwe natafuta ufadhili wa elimu niko darasa la tatu ninaahidi kujituma katika kusoma kwa mawasiliano 0714464124 au 0627075311

    ReplyDelete
  2. Naitwa mariam honero nina stashahada ya uhasibu natafuta mfadhiri wa kunisaidia kulipa ada ili niweze kufikia malengo yangu. Kwa mawasiliano +255786133403 au +255716559896

    ReplyDelete
  3. Naitwa victor natafuta mfathili was kunilipia ada ya ngazi ya diploma kwa mawasiliano victorkanza4@gmail.com

    ReplyDelete
  4. Naitwa Fatma natafta mfadhili wa masomo kwa ngazi ya Degree.
    Tafadhali 0714783802

    ReplyDelete
  5. Mimi naitwa Teresia Luhwago nimehitimu diploma ya maendeleo ya jamii naomba msaada wa kusomeshwa dgree ya maendeleo ya jamii naahidi sito muangusha atakaye nisaidia.mawasiliano 0762423348,0625430820

    ReplyDelete
  6. Naitwa Teresia Luhwago nimehitimu diploma ya maendeleo ya jamii naomba msaada wa kusomeshwa ngazi ya dgree kwa kada ya maendeleo ya jamii.mawasiliano 0762423348,0625430820, telesialuhwago20@gmail.com

    ReplyDelete
  7. Naitwa Anyawile Eliud ninaomba msaada wa mtaji wa kilimo cha matunda

    ReplyDelete
  8. Naitwa ajuaye katanyele naomba msaada wa mtaji wa biashara ya nguo na mungu atakubariki 0765632335 katanyeleajuaye@gmail.com

    ReplyDelete
  9. Naitwa Neema kalei nahitaji ufadhili wa kusomesha watoto wangu.0621105032

    ReplyDelete
  10. Naitwa Hassan Albaswari.. Naitaji wafadhili watu s aidie kwa ni tu naleya Mayatima...Allah iko pamoja daaima na wale wanaojitolea pesa za o kwa ajili ya Allah+25769881874

    ReplyDelete