FAIDA UNAZOKOSA KWA KUTOTAJA VYANZO VYA HABARI AU PICHA ZAKO

Imekuwa ni kasumba watu wengi kutumia status, inspirational quotes, makala au picha za wenzao katika websites zao, blogs zao au hata kwa kupost kama status za Facebook bila kuwataja wahusika wenyewe walioandaa kwa mara ya kwanza post husika. Makala hii itakueleza faida unazo kosa kwa kutotaja wamiliki haswa wa habari au picha husika.
Wapo wengi wafanyao hivyo tena bila aibu huandika au kupost kama ilivyo, isipokuwa wanajifanya wao ndio walioandika wakati kiukweli  ni COPY AND PASTE. Posts nyingi za Mbuke Times zimekuwa zikitumika kwa blogs na hata kurasa za Facebook bila hata Mbuke Times kutajwa. Hizi hapa:-
1. Hii ipo kwa Facebook bofya hapa
2. Tena akapost kwa blogu yake bofya hapa
3. Hii ni status yangu ya Kurasa ya Mbuke Times FB ila imetokea kwa blog hii bofya hapa
4. Hii wameipost kwa Facebook. bofya hapa
Hata hivyo ni MUHIMU KUJUA KUWA
Kutaja chanzo cha habari, taarifa au somo unaloandika katika blogu yako lina faida kubwa sana kwako wewe mwenyewe zaidi ya unavyoweza kudhani. Zifuatazo ni baadhi ya faida:-
1. Kushinda roho ya ubinafsi hivyo kujijengea mazoea ya kufikiri vema na uhuru wa fikra. Wengi wanaacha kutaja blogs au website za wengine kwa sababu tuu wanaona watawanufaisha wenzao kwa kuwa wengine watajua wapi makala husika ilikuwepo hapo mwanzo. Fikra za ubinafsi na roho ya kwanini kama hiyo zinaonyesha wazi kuwa mtazamo wako wa maisha ni finyu kwani wewe kuwa juu si lazima wengine wawe chini. Furaha yako haitegemei kwamba wengine eti wawe na huzuni.
2. Kutaja vyombo vingine vya habari au watu ni jambo jema kwako katika kujenga ushirikiano. Watu husika au vyombo vingine vikigundua kuwa umewavitaja au umewataja inakujengea heshima na urafiki nao. Hivyo nao wanaweza tumia picha, makala zako na kukutaja pia.
3. Kujijengea heshima na uaminifu kwa wasomaji wako: Pale wasomaji wako wanaposoma na kuona umetaja vyanzo mbalimbali vya unayoandika, inasaidia kuwafanya wakuamini zaidi na kukuona mtu mwenye kufanya utafiti wa unayoandika. Pia wanakuona kuwa ni mtu mwenye kupenda ushirikiano na mwenye kujali na kuheshimu kazi za wengine. Kumbuka imani ya wasomaji wako ni muhimu sana ili waendelee kuja kusoma makala au posts zako.
Hata hivyo kumbuka kuwa pamoja na kutaja wapi umetoa picha au makala yako, kuna wakati kufanya hivyo tuu haitoshi unahitaji :-
A: Kuomba ruhusa ya mmiliki wa makala au picha husika kwani makala au picha nyingine zina masharti hayo ya hakimiliki.
B: Kutokubadili maneno fulani yanayokuja na makala au picha husika. Hii pia ipo kwa TEMPLATES za bure unazozipata kwa ajili ya kutumia kwa website au blog yako.
Maelezo haya ni sehemu ya tafakari toka website ya ABOUT US.COM katika makala zao hizi mbili.Kusoma  BOFYA HAPA au HAPA.
Share:

0 comments:

Post a Comment