Ni jambo la busara kuwa na vyanzo tofauti vya mapato. Haijalishi aina gani ya kazi uliyo nayo au kiwango chako cha elimu, blog inaweza kuwa chanzo chako cha mapato endapo utaifanya kwa umakini na kwa kujipanga.
Ninasema kama utaifanya kwa umakini na kwa kujipanga kwakua sio kila mwenye blog basi inamuingizia fedha. Wengi haswa walioanzisha blog kwa kuiga , kutaka matokeo ya haraka haraka , na bila kuwa na mkakati mathubuti na wa muda mrefu hawajafanikiwa na pengine wengi wao wameishia njiani.
Kuandikisha blog na kuiremba kwa muonekano ni jambo la msingi, ila kufahamu na kuweza kuiendesha ili kweli ikuletee kipato ni jambo tofauti na gumu zaidi linalohitaji kujipanga kweli kweli.
Katika makala hii ninakuelezea mambo ya msingi ya kuzingatia ili kweli blog ikuletee faida ya kifedha kama biashara, na kwa kufanya hivyo bila shaka utapata faida nyingine za kukua wewe kama wewe, kiufahamu na kimaendeleo yako binafsi.
1. Kutambua haswa namna kuingiza hela:
Kuna namna tofauti ambapo blog inaweza kukuingizia hela. Mfano waweza ingiza hela kupitia matangazo kwa blog yako. Nyingine ni kuwa kupitia blog yako na makala zako ukatambulika wewe kama mjuzi wa aina fulani na hivyo ukaingiza hela kwa kupitia huduma zako utakazotoa, au bidhaa ambazo utauza kwakua tayari umeshafahamika na kuaminika wewe ni wa aina gani.
Mfano,mapato ya Mbuke Times si kama wengi wanavyotarajia kuwa kipato cha blog kitoke katika MATANGAZO.
Utaona kuwa Mbuke Times haina matangazo ya biashara. Badala yake mie nimejikita katika kuwahudumia watu kupitia makala zangu, na watu hunitafuta niwahudumie kwa kazi zao mfano za kutengeneza website, kufundisha English, au kujipatia vitabu ambavyo nimeandika. Pia kama mshauri wa mambo ya biashara, wengi hunitafuta kwakua wanasoma makala zangu za ujasiriamali hapa Mbuke Times.
Wakati mwingine vyombo vya habari hunitafuta ili wanilipe niwapatie makala. Kwahiyo aina yangu ya kuingiza kipato niliyoichagua zaidi ni kuwafikia watu moja kwa moja ambao watafaidika na kuhitaji ujuzi wangu, na sio watu wa matangazo, ingawaje ikitokea kupata matangazo nitapokea.
Sio lazima ufanye kama mie. Kuna njia nyingi za kuingiza hela kupitia blog kama vile matangazo ya biashara, adsense, na kuuza bidhaa za watu wengine kupitia blog yako.
Mfano,mapato ya Mbuke Times si kama wengi wanavyotarajia kuwa kipato cha blog kitoke katika MATANGAZO.
Utaona kuwa Mbuke Times haina matangazo ya biashara. Badala yake mie nimejikita katika kuwahudumia watu kupitia makala zangu, na watu hunitafuta niwahudumie kwa kazi zao mfano za kutengeneza website, kufundisha English, au kujipatia vitabu ambavyo nimeandika. Pia kama mshauri wa mambo ya biashara, wengi hunitafuta kwakua wanasoma makala zangu za ujasiriamali hapa Mbuke Times.
Wakati mwingine vyombo vya habari hunitafuta ili wanilipe niwapatie makala. Kwahiyo aina yangu ya kuingiza kipato niliyoichagua zaidi ni kuwafikia watu moja kwa moja ambao watafaidika na kuhitaji ujuzi wangu, na sio watu wa matangazo, ingawaje ikitokea kupata matangazo nitapokea.
Sio lazima ufanye kama mie. Kuna njia nyingi za kuingiza hela kupitia blog kama vile matangazo ya biashara, adsense, na kuuza bidhaa za watu wengine kupitia blog yako.
![]() |
| Hii ni sehemu ya makala zangu nilizotoa kwa gazeti la Mwananchi |
2. Kutambua walengwa haswa ni akina nani:
Point hii inaendana na point ya hapo juu ya kutambua namna gani unataka kuingiza hela kupitia blog. Ukishajua aina gani unataka kuingiza kipato kupitia blog, basi itakupasa uchambue kwa umakini ni akina nani haswa unawalenga kuwa ndio wawe wasomaji wa blog yako.
Kujua aina ya wasomaji wako kutakufanya ujipange vema kuhusu aina ya lugha utakayoitumia kuandika blog yako, aina ya makala za kuandika , namna ya kuandika makala zako. Nikupe mfano, mie nilichagua siku nyingi aina za walengwa wa blog yangu ndio maana unaona makala zangu ni ndefu na zina aina fulani ya uandishi ambayo huwezi ikuta kwa kila aina ya blog.
Kama umesoma hii makala hadi hapa , basi wewe ni mmoja wa walengwa wangu, na ukijiuliza kwa umakini utaona unakidhi sifa zifuatazo: Unapenda maendeleo kwa sana, unatamani kuwa zaidi ya hapo ulipo, unaamini unahitaji kitu fulani cha zaidi -maarifa ili ukue zaidi, kikwazo chako kikubwa katika kupiga hatua ya juu kimaisha ni mbinu, fikra, namna ya kujipanga, ujuzi zaidi na unahitaji sana muongozo wa mtu anayejua jambo fulani kwa upana.
Ndio maana unaona makala zangu nyingi katika Mbuke Times, zinalenga kujibu hizo shida zako au kukusiliza na kukufikia kwa namna hiyo.
3. Itachukua muda :
Kumbuka kuwa itachukua muda mrefu kutambulika na kujijengea wafuasi ambao watapenda kusoma blog yako mara kwa mara. Siri kubwa ya kuwa na blog yenye kukuingizia kipato ni kupata watu watakaoamini unayoandika, watakaopenda kurudi kusoma mara kwa mara, na ambao watajisikia kuunganika nawe, na hata waweze kukutambulisha kwa watu wengine.
Hivyo basi uwe na mkakati wa kuendelea kutoa makala za mara kwa mara kwa muda mrefu ili kweli watu waifahamu na kuikumbuka blog yako.
4. Kuandika mara kwa mara:
Point hii inaendana na point hapo juu kuwa inakupasa uandike mara kwa mara makala nyingi, kama ukishinda kabisa basi walau mara tatu kwa wiki.
![]() |
| Kuandika makala nzuri huchukua muda na huhitaji umakini wa hali ya juu na utafiti |
5. Hakikisha unajitangaza:
Kuwa na blog ya kupendeza na makala nyingi nzuri hakutoshi kama watu wengi hawaifahamu biashara yako.
Tumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram, Google+ kujitangaza. Angalizo usiweke matangazo yako huko kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba uwakere watu. Usiwawekee links za blog yako sehemu ambayo haihusiki. Kwanza utajishushia heshima na kuonekana mbabaishaji. Mfano kwenye group la mambo ya siasa, wewe unaweka makala ya blog yako ya ushauri wa mambo ya mapenzi.
6. Kuwa na utambulisho maalum (Brand):
Sio kwa sababu Michuzi anaandika habari za matukio na anapata matangazo mengi basi na wewe ni lazima uingie kuandika habari za matukio.La msingi katika unasiriamali ni kutambua haswa haswa ni tatizo lipi haswa linawakabili watu, na wewe utaweza kulitatua kwa namna gani.
Jijengee kufahamika kwa kutengeneza muonekano wako binafsi na wa blog kiasi kwamba hao watakaosoma blog yako, posts zako katika mitandao ya kijamii kweli wakuamini na wakuone wewe ni wa aina ambayo kweli unaweza saidia, haubagui, unaheshimu wote, na kweli una maaanisha na kuendana na hicho unachoandika.
Angalizo epuka lugha za udhalilishaji, au ambazo zitatafsirika kuwa unadharau au kuwaangalia watu wa aina fulani kwa ubaya mfano, epuka posts ambazo zitatafsirika kama dharau kwa jinsia fulani, dini fulani, au aina fulani ya watu katika jamii kwani yawezekana kabisa hao unaowalenga katika blog yako wanatoka katika kundi husika unalolionyesha dharau.
7. Kuwasiliana na walengwa wako:
Unahitaji kuwa karibu na wasomaji wako kwani kuwa na blog ni kutoa huduma. Wasomaji wako watakuongelesha kupitia comments watakazoacha kwa blog yako, au kupitia akaunti zako za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram au WhatsApp.
Wewe mwenyewe pia unaweza kuanzisha mazungumzo nao kupitia kuwaomba wajaza fomu maalum utakazowauliza maswali.
La msingi ni kukumbuka kuwa unaanzisha blog ili uguse watu kwa namna fulani kupitia makala yako. Unapoanza kufanya uchunguzi na kuandika makala kwa umakini, unajenga imani kwa watu na watu wanategemea kukusikiliza zaidi na kutatua yale yanayowasibu. Hivyo kuwa nao karibu kwa kuwasiliana nao ni jambo la msingi.
8. Kuchambua muelekeo wa blog yako:
Ni vema mara kwa mara kujua haswa haswa blog yako inaelekea vipi, aina gani ya watu wanasoma blog yako, wanasoma wakitokea wapi, ni aina gani haswa za posts zinasomwa , aina gani za posts zinapata likes nyingi au kuwa shared au watu kucomment.
9. Ifanye blog yako ipatikane kupitia Google:
Ili upate watu wengi zaidi kufika kwa blog yako unahitaji kuandika na kuandaa blog yako kiasi kwamba mitandao ambayo husaidia watu kupata taarifa mtandaoni iweze kupata taarifa zako. Hapa nazungumzia kuwa iwe rahisi mtu akisearch kitu fulani kwa Google, basi Google imuonyeshe blog yako. Mbinu hii maalum ya kufanya blog yako iwafikie watu wanaosearch huitwa kwa kitaalamu SEARCH ENGINE OPTIMIZATION (SEO).
Mfano watu wengi waliokuja kwa blog yangu ya Mbuke Times na nikawahudumia, ni kwa sababu walikua wanasearch mambo fulani kwa Google mfano wengine wameniambia walikua wanasearch kuhusu kujifunza English , ndio wakaona Google imewaambia kuhusu Mbuke Times.
| Mfano wa jinsi mtu anavyoweza kusearch akaiona blog yako hapo mtu anasearch jinsi ya kujifunza English na Mbuke Times inaonekana katika majibu. Unaweza kufikia hivi kwa kitu tunachoita SEO |
Hitimisho na ANGALIZO
Yote hayo yanawezakana endapo utaanza vema na kuchambua aina gani ya posts au blog unataka kuwa nayo na akina nani haswa unawalenga. Makala hii ni kwa ajili tuu ya maelezo ya jumla si kama ushauri binafsi.
Kama unahitaji ushauri binafsi na msaada zaidi wa jinsi ya kuchambua wazo lako la blog, kusaidiwa jinsi ya kuandikisha na kutengeneza blog yako ipendeze, au kujua namna ya kuandika makala zitakazopendwa au kuchambua muelekeo wa blog yako, tafadhali wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa email john.myungire@gmail.com
Nitafute pia ili nikusaidie jinsi ya kufanya SEO kwa blog yako na namna ya kutengeneza BRAND.



Ok kaka naomba unielekeze zaidi kuhusu SEO
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteNielekeze kuhusu hiyo Seo
ReplyDeleteNaomba nione malala mbalimbali ya blogi
ReplyDeleteSawa
ReplyDeleteMina olen Bryan Roland ja tahan selle meediumi abil hoiatada kõiki laenutaotlejaid ettevaatlikkuse eest, sest pettusi leidub kõikjal. Mitu kuud tagasi olin rahaliselt stressis ja meeleheite tõttu pettis mind mitu internetilaenuandjat.
ReplyDeleteKaotasin lootuse, kuni mu sõber võttis minuga ühendust ja pakkus välja väga usaldusväärse laenufirma nimega Loan Credit Institutions, kes mind aitas. Nad andsid mulle 145 000 euro suuruse laenu vähem kui 72 tunniga ilma igasuguse stressita. Seega, kui vajate kiiresti laenu, võtke nendega ühendust ja saate laenu neilt. Nad on 100% kindlad ja garanteeritud. Võtke nendega ühendust e-posti teel: loancreditinstitutions00@gmail.com
WhatsApp: +393509313766
Kasutan seda meediumi, et hoiatada kõiki laenutaotlejaid põrgu eest, mida ma nende võltslaenuandjatega läbi elasin. Seega võtke ühendust selle päris laenufirmaga, et saaksite oma laenu kätte ja saaksite sama õnnelikuks kui mina.
Tänan teid ja jumal õnnistagu laenuandjaid!
WhatsApp: +393512114999
Tervitused,
ReplyDeleteMinu nimi on Ana Ahmed ja ma tahan seda kanalit kasutada, et soovitada kõigil olla ettevaatlikud internetis laenu saamisel. Paljud laenuandjad on siin petised ja nende ainus eesmärk on teilt kogu raha välja petta. Taotlesin Saksamaal ühelt naiselt 25 000 euro suurust laenu ja kaotasin alguses umbes 1300 eurot. Laenu võtmata küsisid nad minult uuesti lisakulude eest. Maksin peaaegu 3000 eurot ja ikkagi ei saanud ma laenu.
Jumal tänatud, et kohtasin sõpra, kes just taotles laenu ja sai laenu ilma igasuguse stressita. Ta julgustas mind seda taotlema. Taotlesin laenu krediidiasutustelt ja sain 25 000 euro suuruse laenu, mida ma palusin. Alguses arvasin, et see on nali ja pettus, kuid sain laenu vähem kui 72 tunniga ja 3% intressimääraga ilma tagatiseta. Olen väga õnnelik, et olen vaesusest pääsenud.
Seega soovitan kõigil, kes vajavad laenu, võtta ühendust laenuandjatega e-posti teel: (loancreditinstitutions00@gmail.com) või WhatsAppi teel: +393512114999. Lisateabe saamiseks võite nendega ühendust võtta ka WhatsAppi teel: +393509313766.
Tere kõigile
ReplyDeleteMinu nimi on Alexandru Avram Codrin ja ma olen pärit Rumeeniast. Tahan öelda kõigile laenutaotlejatele, et on ainult üks päris laenufirma, mis pakub laene, ja nad aitasid mind 15 000 euro suuruse laenuga. Ettevõte on Loan Credit Institutions ja see laenuandja aitas mind laenuga, tema nimi on hr Elijah, seega kui teil on vaja laenu, minge kohe sellesse ettevõttesse ja saage oma laen sealt. Laenud on turvalised ja kiired. Nende e-posti aadress on loancreditinstitutions00@gmail.com. Seega soovin teile, laenutaotlejad, kõike head. See on päris ettevõte, mis pakub laene.
E-post: loancreditinstitutions00@gmail.com
WhatsApp: +393512114999
WhatsApp: +393509313766
Tere kõigile
ReplyDeleteMinu nimi on Anastasia Sofia, olen pärit Leedust ja elan Leedu pealinnas Vilniuses. Otsisin internetist laenu ja sain ainult pettureid, aga leidsin laenufirma nimega Loan Credit Institutions ja nägin internetis inimesi tunnistamas nende heategusid. Seega otsustasin proovida, kas olen jälle õnnelik. Taotlesin 60 000 euro suurust laenu ja laenuandja hr Elijah kinnitas mulle, et 5 päeva pärast on mu laen minu pangakontol. Täna, kui ma töötasin, sain pangast teate, et mu kontol on 60 000 eurot. Tänan Loan Credit Institutionsi aususe eest. Kui vajate veebilaenu, siis kandideerige sellelt ettevõttelt, sest see on ainus päris ettevõte, mis pakub veebilaene. Nende e-posti aadress on loancreditinstitutions00@gmail.com. Kuid saate nendega siiski WhatsAppi kaudu ühendust võtta, kuna nad kasutavad kahte erinevat WhatsAppi numbrit. Nende WhatsAppi kontaktandmed on järgmised: +393512114999. või +393509313766.
Tere kõigile, minu nimi on Vlad Toma. Olen pärit Bukarestist, Rumeeniast. Kuulsin ettevõttest nimega Loan Credit Institutions, mis aitab inimesi laenudega üle kogu maailma. Otsisin kord internetist laenu ja mind pettis kaks võltsitud ettevõtet. Pärast seda ei uskunud ma enam kunagi, et internetist võib leida head laenuandjat. Arvasin, et nad kõik on petised, kuni leidsin ettevõtte nimega Loan Credit Institutions. Leidsin inimesi, kes selle ettevõtte kohta tunnistusi andsid, ja olin üllatunud, miks ma seda ettevõtet õigel ajal ei leidnud. Ma ei uskunud kunagi seda, mida inimesed ettevõtte kohta rääkisid, kuni ma ise avalduse esitasin ja neid proovisin. Summa, mida otsisin, oli suur ja see oli kinnisvara jaoks. Laenusumma oli 850 000 eurot. Seega esitasin avalduse ja härra Elijah rääkis minuga, kuid arvestades minu suurt laenu, kulus laenu saamiseks vaid 7 tööpäeva. Ainus, mida ta mulle käskis teha, oli pangaülekande tasu, mida pank kavatseb kasutada minu laenu minu pangakontole kandmiseks, kui ta mulle ütles, et kartsin, et see on pettus, aga ma ütlesin, et proovi järele. Kandsin ülekandetasu, mis oli deklareeritud ja mis laekus kokku vähem kui 7 tööpäeva jooksul. Sain oma pangast teate, et 850 000 eurot kanti minu pangakontole ja kõik raha kohta, üksikasjad ja see, kellelt see tuli, olid laenuandjad, kes mind aitasid, kui ma seda esimest korda nägin. Olin üllatunud, et ma ei uskunud oma silmi, aga see oli tõsi. Nii et ma ütlesin endale, teiste inimeste sõnul aitas ettevõte mind heategude tunnistajana. Lasin endal seda teha, sest minu arvates pole tänapäeval lihtne leida seaduslikku veebilaenu pakkuvat ettevõtet, seega peaks igaüks, kes vajab veebilaenu ilma pettuseta, kandideerima just sellelt ettevõttelt, sest see on ainus, millega nad teid aidata saavad. Ma kinnitasin seda ja on tõsi, et olen nii õnnelik ja tean, et see ettevõte teeb veelgi rohkem inimesi õnnelikumaks kui mina. Selle ettevõttega saab ühendust võtta e-posti või WhatsAppi teel, aga mina kasutasin WhatsAppi, kuna see oli kiirem. Ettevõtte e-posti aadress on loancreditinstitutions00@gmail.com ja WhatsAppi aadress on +393509313766 või +393512114999. Tänan teid kõiki, tervitused Vlad Tomalt Bukarestist, Rumeeniast.
ReplyDelete