ZAMBIA WATUMIA FEDHA ILIYOPUNGUZWA SIFURI TATU

Picha na website ya benki kuu ya Zambia
**Mpya**PICHA ADIMU
Kama kawaida kila ijumaa huwa nawaletea picha ya kitu, tukio au habari yenye upekee fulani. Leo ni picha ya fedha ya Zambia. Zambia wameamua kuondoa SIFURI katika sarafu zao ili kuondoka na tatizo la kuwa na fedha zenye namba kubwa. 
Mfano pichani ELFU TANO, inakuwa TANO. 


Nilipokuwa Zambia mwaka 2011 nilisikia habari hii, ila sasa fedha hizi zimeanza kutumika rasmi na wenye fedha zote za zamani hawawezi kuzitumia mpaka wakabadilishe benki.



 Rafiki yangu aliyepo Zambia amenithibitishia hili la kuanza rasmi kutumia Kwacha zilizopunguzwa sifuri tatu. 
Share:

0 comments:

Post a Comment