RAHISISHA NA KUWA NA UFANISI KATIKA KUTUMIA KOMPYUTA KWA MBINU HIZI

Leo tunaendelea na makala yetu ya jinsi ya kuwa mfanisi wakati wa kutumia kompyuta.

2. Matumizi sahihi ya Folders
Hifadhi picha na files nyingine katika folders ili iwe rahisi kujua wapi file husika lipo. Hata hivyo haitoshi tuu kuwa na folders , jitahidi folders husika uzipe majina ambayo yatakusaidia kweli kujua folder husika linahusu nini.  Waweza pia tengeneza folders ndani ya folders ili iwe rahisi kujumuisha files zako sehemu moja katika kila folder ndogo ndogo. Mfano: Unaweza kuwa na folder la BURUDANI. Ndani ya folder hilo la burudani ukaweka foldes nyingine ndogo ndogo kama vile folder la MOVIES, folder la AUDIO, folder la VIDEO. Kutegemea na wingi wa files zako unaweza pia kuyagawa hata hizo folders ndogo ndogo katika folders nyingine ili kurahisisha zaidi utafutaji wa files zako. Yaani mfano ndani ya folder la AUDIO ukatengeneza tena folder la BONGO FLEVA, BLUES, n.k

3. Igawe screen ya kompyuta

Unaweza kuigawa screen ya kompyuta yako katika sehemu mbili au hata zaidi kwa kuelekeza kuwa SHOW WINDOWS SIDE BY SIDE kwa wenye windows 7. Kama hautumii windows7 basi angalia hapo hapo chini kwenye Task Bar uone neno linaloendana na kugawa screen -kama TILE WINDOWS VERTICALLY.
Kugawa screen yako nenda sehemu iliyo wazi ya task bar, kisha right click mouse, utaona options kama hizo hapo pichani. Kuondoa huko kugawanywa kwa screen , fanya kama ulivyofanya hapo juu yaani nenda sehemu iliyo wazi ya task bar, kisha right click mouse, utaona options ya UNDO WINDOWS SIDE BY SIDE.

4. Tafuta na pata kwa haraka folders na files kwa kompyuta yako.
Wakati mwingine unaweza ku search tuu folder au file husika kwa kutumia sehemu maalum ya kompyuta yako inayokuwezesha kusearch. Andika jina la file au folder la  unachotaka kufungua moja kwa moja utaletewa uchaguzi mbalimbali kama unavyoona katika picha.

5. Ku copy na Ku paste badala ya ku-type
Jaribu kadri iwezekanavyo kutokutype badala yake u copy maneno husika unayoyataka kama yameandikwa sehemu nyingine, na kupaste katika document unayoifanyia kazi. Hata kama maneno husika hayapo kama utakavyo, kwamba unahitaji kurekebisha kidogo, ni vema uka copy na kupaste kisha ukarekebisha hayo uliyo kwisha  paste. 

6: Jifunze kutumia shortcuts mbalimbali ili kurahisisha kazi zako 
Mfano wa shortcuts ambazo utazitumia mara kwa mara ni CTRL+C  kwa ajili ya ku copy, na CTRL+V kwa ajili ya ku paste. Nyingine ni CTRL+B = kubold maandishi, na CTRL+F kutafuta maneno. Wakati CTRL+Z kurudi hatua moja nyuma ( ku UNDO). CTRL+A = Select All.
Search hapa mtandaoni kwa kutumia GOOGLE kujua shortcuts nyingine nyingi unazoweza kutumia kurahisisha kazi zako.
Kwa kusearch neno cape ninapatiwa files mbalimbali na folder zinazoanza na herufi C.
Share:

1 comment: