JINSI YA KURAHISISHA MATUMIZI YAKO YA KOMPYUTA


MUHIMU KUJUA KUWA
Waweza tumia njia zifuatazo ili kufanya matumizi yako ya kompyuta yawe ya ufanisi:
1. Tumia CTRL+F : Yaani kwa keyboard yako ya kompyuta shikiria CTRL na F utaona kijisehemu cha kuandika kimetokea ambacho utaweza kuaindisha kitu unachotaka kukiona katika ukurasa husika kwa haraka.
Mfano upo katika ukurasa huu wa MBUKE TIMES na unataka kwa haraka kusoma post ya KAMA HAUKUJUA BASI JUA, wewe fanya hivi bofya CTRL na F kisha andika hilo neno kama haukujua basi jua, halafu angalia kompyuta yako itakua ikiweka kivuli sehemu neno search yako ilipo. 
Waweza pia kutumia hili kutafuta kichwa cha habari kwa haraka katika document yako ya MS WORD, PDF au hata ukurasa mwingine wa website kama vile unaposoma habari za Wikipedia. Mfano nilipoandika habari ya TAKWIMU ZA AFRIKA kuhusu nchi tajiri na masikini. Mie nilfungua ukurasa wenye kuelezea mambo mengi kuhusu Afrika. Hata hivyo kwa kuwa lengo lilikuwa tuu kujua kuhusu ukubwa na udogo wa nchi za Afrika , nilibofya zangu CTRL+F kisha kuandika biggest country, nikapata kwa haraka nchi kubwa kuliko zote Afrika, halafu nikaandika tena smallest country moja kwa moja nikapelekwa palipoandikwa kuhusu nchi ndogo Afrika.
2. Matumizi sahihi ya FOLDERS. (Soma kesho kwa blog yetu)
3. Igawe screen ya kompyuta yako kwa sehemu mbili au hata tatu.Kadri upendavyo ( Soma hii kesho kwa blog).
4. Tafuta na pata kwa haraka Folders au files kwa kompyuta yako. 
( Soma hii kesho kwa blog).
Share:

0 comments:

Post a Comment