FAHAMU KITU CHA KIPEKEE CHA KUJIFUNZA TOKA KWA PELE

Picha na SCARYFOOTBALL.COM

Haya ni baadhi ya matukio katika SOKA yanayoonyesha kuwa ili kuwa bora inakupasa ujitume kweli kweli, ni kama ujitoe kafara fulani (sacrifice) ili kujitofautisha. Hivi ndivyo PELE alivyojitofautisha na kutambuliwa na watu:-
Katika fainali ya mwaka 1958 Pele ambaye pia ni mchezaji bora wa FIFA wa karne ya 20, alianza rasmi kucheza kombe la Dunia. Wakati huo akiwa na miaka 17. Katika mechi ya fainali mwaka huo 1958 dhidi ya Sweden Pele alifunga magoli mawili,ambapo Brazili ilishinda magoli 5 dhidi ya 2 ya Sweden.
Baada ya kipenga cha mwisho Pele alizimia.
--Kuelezea ufundi na kujituma kwa Pele, mmoja wa wachezaji wa Sweden aliyekuwepo katika kikosi cha 1958 alisema : " Pele alipofunga goli la pili, nilijisikia kuenda kumpongeza /kushangilia".
Fikiria ni kwa jinsi inawezakana mchezaji wa timu pinzani ajihisi kushangilia goli uliloifunga timu yake !
--Ufundi na kujituma kwa Pele kunaelezwa pia na beki wa timu ya taifa ya Italia katika fainali za kombe la dunia mwaka 1970 ambapo anasema : " Kabla ya mechi nilijiambia kuwa Pele ni mtu tuu wa kawaida ana ngozi na damu kama sisi. Ila baadae niligundua nilikuwa nimekosea kuwaza".
Kwa Chanzo: FIFA ambapo waweza soma nukuu kama hizi:-
"Pele is the greatest player of all time. He reigned supreme for 20 years. All the others - Diego Maradona, Johan Cruyff, Michel Platini - rank beneath him. There's no one to compare with Pele. Franz Beckenbauer, West Germany's 1974 FIFA World Cup-winning captain who played alongside Pele for New York Cosmos.

"We felt very good before the tournament. Pele was saying that we were going to win, and if Pele was saying that, then we were going to win the World Cup." Carlos Alberto, Brazil's 1970 FIFA World Cup-winning captain
Share:

0 comments:

Post a Comment