JINSI YA KUJIFUNDISHA ADABU YA MUDA


Ingawa ni kweli kuwa hakuna kanuni ya jumla ya nini ufanye ili ufanikiwe, kumbuka kuna tabia za jumla za watu waliowahi kufanikiwa.

Mojawapo ya muongozo katika kufikia mafanikio unayotamani ni :-
Kutambua wazi wazi ni shughuli gani za muhimu kwako.
Halafu ukazipa kipaumbele hizo shughuli muhimu kwako
Ninaposema kutambua wazi wazi nina maana kuwa kwanza uchukue muda wa kutafakari maisha yako kipindi na kipindi kwani maisha yanabadilika na wewe mwenyewe unabadilika kitabia na kitafakari. Ikiwezekana weka malengo yako katika maandishi.
--Kisha tambua ni shughuli gani unazotakiwa kufanya kufikia malengo hayo, weka bayana sio tuu shughuli gani au mambo gani unatakiwa kufanya, bali pia ujue ni wakati gani unatakiwa kufanya.
--Halafu ujidhibiti wewe mwenyewe kwa kuwa na nidhamu ya kufanya hayo tuu ya msingi kwa wakati husika. Mfano kwa wanafunzi kama upo chuoni, wajua wazi jambo la kwanza kabisa la msingi kwako ni kupata uelewa na maksi nzuri, iweje uwe mtu wa kufuata mkumbo wa mambo mengine yanayokukosesha muda wa kujisomea vema ?
--Kama unafanya kazi basi unajua wazi pengine lengo lako ni kufanya kazi husika kwa muda tuu, kisha ukajiajiri. Iweje ujiingize kwenye majungu na uvivu, na kufuatilia mambo yasiyokujenga kupata ujuzi na uzoefu wa kutosha kuja kujiajiri ?
---Swala la kukumbuka nini haswa la msingi unatakiwa kulifanya au kulipata kwa wakati husika huwashinda wengi. Unakuta umeenda ofisi ya watu, ndio una haraka lakini la msingi zaidi ni wewe upate huduma yao. Kwa sababu ya ubovu wa huduma kwa mteja pengine hawakuhudumii vema, unaanzisha zogo, halafu unaamua kuondoka. Kuondoka kwako kunakugharimu zaidi, ila unajipa moyo eti "UMEWAFUNDISHA ADABU". 
Ingawa kulalamikia huduma mbovu ni jambo la msingi , lakini halikuwa jambo la kupewa kipaumbele na wewe. Kama ulitaka kuwafundisha adabu kwa kuanzisha zogo na kutimka ungeeandaa siku maalum ya kufanya hivyo.
Share:

MAMBO MATANO YA KWELI DUNIANI YATAKAYOKUACHA MDOMO WAZI


KAMA HAUKUJUA BASI JUA KUWA
1. Kwa mujibu wa scientificamerican.com, Mende anaweza kuishi kwa siku TISA bila kuwa na kichwa.

2. Kuna aina ya samaki aitwae STARFISH ambaye samaki huyo hana UBONGO. Kwa mujibu wa Wikipedia

3. Katika misuli ya binadamu, msuli ambao unafanya kazi nyingi na ni imara kuliko yote ni ULIMI kwa mujibu wa livescience.com

4. Tembo,kiboko na kifaru ndio mnyama ambao hawawezi kuruka juu. Hapa kuruka ina maana kuwa na miguu yao yote juu. Kwa mujibu wa listverse.com

5. Kwa mujibu wa scienceline.ucsb.edu wanyama wengi ukiacha binadamu na dolphin hufanya mapenzi ili tuu waweze kuzaliana. Hivyo kwa wanyama wengine kama hakuna dalili kuwa mnyama wa kike hatopata ujauzito , basi wanyama hao hawafanyi mapenzi. Mojawapo ya dalili kuwa mnyama anaweza kubeba ujauzito ni kutoa aina fulani ya harufu, sauti, na hata kubadilika muonekano wake ili kutoa ishara kwa mnyama mwanaume.
Share:

FAHAMU JINSI YA KUTAMBUA BAHATI


Tafakari yetu leo inahusu BAHATI
Ni kweli kuwa kuna kufanya bidii ili kufanikiwa, hata hivyo sio kila mafanikio yako basi ni kwa sababu ya juhudi zako. Basi tuseme yale ambayo yametokea kwa maisha yako bila wewe kuweka mipango au juhudi, basi hiyo ni bahati.
Wakati mwingne waweza kweli kuweka mipango na juhudi lakini ukapata matokeo ambayo ni zaidi ya hizo juhudi au mipango yako.Hiyo nayo ni bahati.
Kuna mambo mengine yapo wazi kabisa, mfano kuwa mzuri wa sura au umbo, kuwa wa kabila fulani, nchi fulani , wa mkoa fulani, na hata kuzaliwa katika familia fulani yote zote hizo ni bahati.

Mengine ya kukumbuka ya msingi kuhusu bahati ni kuwa:-
1. Ukitambua uwepo wa bahati mbalimbali ulizonazo utakuwa mnyenyekevu (usiye na makuu) na utaheshimu na kuthamini wengine ambao wana hali ya chini kwa kujilinganisha nao.
2. Bahati nyingine zinajitokeza kwa sababu ya juhudi binafsi na mipango pia. Mfano kwa juhudi zako za kufanya kazi vema, unapata bahati ya kukutana na bosi au wateja ambao wanakupatia dili kubwa zaidi ya kukutoa kimaisha. Nasema bahati kwakuwa sio kila mtu mwenye kufanya kazi kwa bidii na uaminifu atapata watu wa kumpa dili kubwa kubwa.
3. Kuna nyakati ili bahati ilete maana katika maisha yako ni lazima uwe umejiandaa kuitumia bahati husika, na hata ikiwepo ni lazima ufanye kazi kuilinda. Ndio maana wapo watoto wa matajiri wanakuja kuishi maisha ya kifukara, wapo waliobahatika kuwa watu maarufu ila wameshindwa kuutumia umaarufu wao kujiletea maendeleo. Wapo baadhi waliobahatika kuichezea timu ya taifa ungedhani pengine wangejibidiisha ili waonekane kimataifa, ila wameridhika na klabu zao.
Share:

JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 5

VERB TO BE
Jinsi ya kuelezea namna watu au vitu vilivyo: ( TO BE), na ili kuelezea hali kwa mfano:-
Huyu huwa mgonjwa daima
Yule yupo makini kila siku
Sisi ni watu wa furaha siku zote.
Huwa tunatumia  AM, IS na ARE) kwa simple present tense.
Umeshasoma jinsi ya kutumia AM, IS na ARE ila kumbuka ulijifunza kutumia hizo AM, IS  na ARE pamoja na vitendo mfano ulijifunza kusema HE  IS READING (Anasoma), WE ARE NOT COMING (Sisi hatuji).
Ni vema ukajua utofauti wa IS, ARE, AM kama verb to be, na  wakati ambapo tunazitumia kuunganisha na vitendo. Umeona kuwa IS, ARE , AM zikitumika na vitendo lazima vitendo viwe na ING, mfano He IS reading.
Hata hivyo tunapozungumza IS , ARE , na AM kama Verb To katika simper present tense, hapa hatuhusishi vitendo. Mfano
He is always careful. ( Daima yupo makini)
We are always happy people. (Sisi ni watu wa furaha siku zote.)
Daima nipo mwenye huzuni. ( I am always sad)


ACTIVE VOICE and PASSIVE VOICE:
Unapotunga sentensi una uchaguzi wa kuanza na mtendaji wa tendo kama vile

John huandika barua.( John is writes letters)- Hapa mtendaji ni John, na anachokitenda ni BARUA.
Mtindo huu wa kuanza na mtenda wa tukio , tunaita ACTIVE VOICE.


Hata hivyo unaweza pia kuamua kuanza na Mtendwa, mfano:
Barua huandikwa na John ( A letter is written by John).
Wao hufundishwa na Issa( They are taught by Issa).
Mie huitwa John. ( I am called John)
Mtindo huu wa kuanza na mtendwa wa tukio , tunaita PASSIVE VOICE

Umegundua nini ?
Ni kwamba kama unaanza na mtendewa wa tendo basi ni lazima utumie neno AM, IS au ARE, halafu kitendo kibadilishwe kiwe katika mtindo tuuitao Past Participle. 
Mfano:
WRITE inakuwa WRITTEN,  
Teach inakuwa TAUGHT n.k. 
Call inakuwa CALLED.

Tafadhali BOFYA HAPA kudownload orodha ya vitendo na past participle zake


Share:

KWANINI KILA JAMBO LINA FAIDA ILA WEWE TUU HUIONI


Kuna mtu ameniuliza swali mbona Mbuke Times haina matangazo ya biashara sasa ninapataje faida ? Si ni bora niache kwa kuwa ni kama napoteza muda wangu na nguvu zangu.
Akanikumbusha nizungumze kasumba ambayo mara nyingi watu wengi wanayo ambayo ni kuangalia faida ya kifedha, tena hela inayoingia wakati huo huo au ndani ya muda mfupi ujao.



Yawezekana hauna tabia ya kufikiria namna ya kutengeneza faida ya baadae, inawezekana mtazamo wako ni wa aina moja tuu kuhusu unavyoweza kunufaika na jambo fulani.



Itazame faida kwa namna hii:-
1. Inawezekana fadia kweli ya hela ikaingia baadae sio lazima sasa.
2. Inawezekana ukapata fedha kwa njia tofauti na hiyo unayodhani lakini hiyo njia nyingine ni kwa sababu ya hilo jambo ambalo unadhani halina faida.
3. Faida sio lazima iwe fedha, kwan hata kukutana na watu wengine, wewe mwenyewe kujifunza mambo, kupata uzoefu wa shughuli husika, na pengine katka kufanya hivyo ukachochewa kujishughulisha na jambo lingine zaidi. Mfano kuandika kwangu blog , kumenichochea kusoma IT kwa nguvu zote. Hii ni faida ambayo siwezi kuipima kifedha.
--Shughuli za NGOs na kujitolea zimenipa fikra pana za kimaisha kwani unapofanya kazi na watu wasiojiweza kimwili na kifedha unapata kujua namna maisha yalivyo kwa upana zaidi.


HIVYO ACHA KUAHIRISHA KUFANYA MAMBO YA MSINGI , eti kwa sababu HAUONI FAIDA. Mtu mwingine hata kujisomea tuu atasema haoni faida, kwani anasema anasubiri apate kusoma ambako kutampata CHETI. Yaani kwake KUJIELIMISHA kusiko na cheti huko HAKUNA FAIDA.
Share:

STORI ISIYOELEZWA NA WENGI KUHUSU DIDIER DROGBA..

Picha na moonofthesouth.com
Katika mahojiano yake  na kituo cha runinga cha ITV, yaliyorushwa hewani tarehe 10/12/2013  Didier Drogba alizungumzia hivi kuhusu kuhamia kwake Uingereza toka timu iliyompatia umaarufu nchini Ufaransa ya Olympique Marseille

“Yeah there was some moments when I was saying maybe it’s not for me. Maybe I go back to France, I go back to Marseille because I still had that feeling for Marseille but then I’m you know, I’m a fighter and I was like, ‘No, I came here and I need to achieve something, I need to achieve something and I need to make history here.’ 

Yaani :
Kuna nyakati nilikuwa nasema kuwa pengine hii sio kwa ajili yangu. Labda tuu nirudi Ufaransa, nirudi Marseille kwa sababu bado nilikuwa naipenda Marseille, ila wajua, mie ni mpiganaji, na nikawa kama, Hapana nilikuja hapa na ninahitaji kufikia kitu fulani.  Nahitaji kufikia kitu fulani, na ninahitaji kuweka historia hapa".

Na Drogba anaeleza hivi kuhusu namna anavyojisikia hususani akirudi kwao Ivory Coast:

“First of all I don’t see myself as a superstar, I see myself as a normal guy, one of these guys who had more chances, who was lucky to have his parents behind him to give him the chance to have a good chance in life. So when I go there I don’t know, I always feel that I was lucky to have met that journey because a lot of them some people are better than me, some of the guys there that are playing are much better than me but they didn’t have the chance I had so I do not see myself as a superstar.”
Yaani: 
" Kwanza kabisa, sijioni kama ni superstar. Najiona kama mtu wa kawaida tuu, mmoja wa hawa (wa Ivory Coast) ambaye alipata nafasi zaidi , mtu ambaye alikuwa mwenye bahati ya kupata wazazi wa kumpa nafasi ya kuwa na nafasi nzuri kimaisha. Hivyo ninapoenda kule (Ivory Coast) , daima hujisikia kuwa ni mtu mwenye bahati ya kukutana na ile safari (ya mafanikio) kwa kuwa wapo wengi kati ya hawa watu (wa Ivory Coast) ambao wanacheza vizuri zaidi yangu, ila hawajapata nafasi kama niliyoipata mie, hivyo sijisikii kama ni superstar".

Embu soma kwa uchache wasifu wa Didier hapa chini:-(kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyonukuliwa na Wikipedia.)
  1. Jina lake kamili ni Didier Yves Drogba Tébily
  2. Didier hakuwahi kucheza katika Soccer Academy yoyote
  3. Alianza mpira wa kulipwa akiwa na miaka 21
  4. Timu yake iliyomtoa - Levallois Sporting Club ya Ufaransa imeupa jina uwanja wake jina la Didier Drogba
  5. Drogba alichangia kutoka mfukoni mwake paundi Milioni 3 alizopata kwa tangazo la Pepsi kwa kujenga hospitali huko nchini kwao Ivory Coast.
  6. Drogba ana asasi yake isiyo ya kiserikali iitwayo  "Didier Drogba Foundation" na katika kumuunga mkono, Chelsea imechangia fedha za kuendesha asasi hiyo. Drogba ndiye Raisi wa asasi hiyo.
  7. May 9,2011 Drogba alisusia kushangilia goli wakati wachezaji wenzake wote walikuwa wakishangilia goli lililofungwa na Frank Lampard kwa njia ya penati.. Kisa ? Eti alitaka apewe yeye afunge ili awe mfungaji bora wa ligi kwani alikuwa amebakiza goli moja tuu kumzidi Wayne Rooney. Hata hivyo katika mechi hiyo ya Chelsea na Wigan Athletic, timu yake ikapata nafasi ya penalti na hapo akaachiwa nafasi naye akashinda na kuwa mfungaji bora wa msimu wa 2010-2011.
  8. Mbali na soka, Didier Drogba ana elimu ya uhasibu.
  9. Drogba ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika historia ya timu ya Taifa ya Ivory Coast.
  10. Drogba pia ndiye mchezaji wa kigeni (mchezaji toka nje ya Uingereza) mwenye magoli mengi zaidi ya kufunga kuliko wachezaji wote wa kigeni.
  11. Drogba alianza kuvaa namba 15 alipohamia Chelsea, hadi pale Damien Duff alipohama Chelsea ndipo akachukua namba 11 aliyokuwa akiitumia Duff. 


Share:

HAYA NDIO UNAYOKOSA KWA KUTOKUSHUKURU KWA UFASAHA..

Yawezekana ikaonekana kama ni jambo dogo sana kushukuru lakini shukrani ya kweli kwa mtu mzima kama wewe sio tuu kusema ahsante, bali shukrani ina maana ya kuwa:-
1. Umethamini ulichopewa
2. Umeiona hisani au huduma ya mtu husika
3. Unatambua kuwa ni jambo jema limekutokea kwamba mtu fulani kakupatia kitu au huduma fulani. Ni kama vile kujinyenyekeza kimoyo moyo na kujiambia kuwa pengine wala haukustahili kufanyiwa hivyo ulivyofanyiwa, au kupatiwa hivyo ulivyopatiwa bali ni kwakuwa imekuwa jambo la kheri kwako kupata ulichopata.

Maana hiyo ya shukrani sio tuu kwamba kwa wale wanaokusaidia au kukupatia vitu BUREE, bali hata kama unalipia , bado unahitaji kushukuru kwani wapo wengi wanaolipia huduma au bidhaa na bado wasipate huduma nzuri au wasipatiwe kile wanachohitaji.

Swala la ahsante sio tuu kwenye biashara. Ahsante ni swala la msingi hata katika mahusiano -mume inabidi amuambie ahsante mke, na mke kwa mume pia kwa sababu hizo hizo.
Watoto kwa wazazi pia.Wanafunzi kwa walimu n.k


Hata kama ni mzazi, mwalimu au mpenzi amekutendea jambo jema, usijione kuwa ni eti ulikuwa na haki ya kutendewa hivyo ulivyotendewa hivyo basi hauna haja ya kushukuru.

Kushukuru kwako kwa ufasaha bila kusanifu, kunamgusa mtu husika hivyo kuna muandaa au kumpa hamasa ya kukutendea jambo jema lingine. Ndio maana wanasema KUSHUKURU NI NAMNA NYINGINE YA KUOMBA.

Utaona kuwa shukrani sahihi inakufanya uthamini ubinadamu, shukrani sahihi inakufanya ujitambue vema na kukumbusha kuwa una thamani kwani mtu mwingine amekujali kufanyia hicho ambacho unasema ahsante.
--Mara baada ya kusema hivyo, napenda niseme ahsante kwako msomaji wa Mbuke Times. Uwepo wako na support yako inanipa nguvu ya kutafakari mambo kila siku. Mie pia ninanufaika.



Share:

JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 4: SIMPLE PRESENT TENSE

Katika somo  la pili (BOFYA HAPA KAMA HAUKULISOMA) tuliona kuwa ili kuelewa tenses yoyote ni muhimu kujua 1. Matumizi ya tense husika 2. Kanuni zinazohusu mabadiliko ya vitendo na 3. Kujua namna mionekano ya sentensi inavyokuwa katika tense husika. (Mionekano ya sentensi nilieleza katika somo la kwanza. BOFYA hapa kama hukusoma somo la kwanza.)
1. Kanuni za muundo wa sentensi katika Simple Present Tense
A: Hakikisha vitendo vinaongezwa es au s kwa viwakilishi hivi SHE, HE , IT.
Mfano:
She likes mangoes .  (Hupendelea maembe.)
He goes to school everyday. (Huenda shule kila siku.)
B: Usiongeze es wala s kwa viwakilishi hivi I, WE, YOU , THEY.
I like mangoes. Mimi hupendelea maembe.
We go to school everyday. Sisi huenda shule kila siku.
C: Kama hautumii viwakilishi katika sentensi yako basi hakikisha unakumbuka kuwa kama mtendaji ni mmoja , ongeza es au s kwa vitendo mfano John plays football.

D: Ila kama watendaji ni wengi basi hakikisha hauongezi es wala s katika vitendo hivyo mfano John and Issa play football.
2. Matumizi ya Simple Present Tense

A. Kuelezea mambo ambayo siku zote ni kweli
Mfano: 
Maji huganda katika nyuzi 0. - Water freezes at 0’C.
Sote tunahitaji upendo. -  We all need love.
Ukimwi unaua. -     AIDS kills.

B: Kuelezea Matendo ambayo sio lazima yawe kweli siku zote, ila yanaonyesha hali ambayo itakuwa hivyo kwa muda mrefu.

Ninaishi Tanzania ( I live in Tanzania).
Unafanya kazi serikalini. (You for the government)
Kuelezea Matendo ambayo ni tabia za watu
Mfano Yeye huamka mapema (  He works up early)
Huwa tunacheza mpira wa miguu kila jioni ( We play soccer every evening)
.
C: Present simple tense hutumiwa katika vitabu na magazeti kuelezea matukio sio lazima yawe ni matendo ya kila siku.
Mfano waweza soma: 
Raisi afariki ( The president dies)
The government closes the road. (Serikali yafunga barabara)
World Cup starts  (Kombe la dunia laanza)
Hata hivyo wapo wenye kufanya makosa na hata katika blogs zao utaona kwa mfano imeandikwa The famous actor died today.
D: Kuelezea matukio yajayo ambayo tayari  imekwisha amriwa au kupangwa kuwa hivyo.
Mfano:  Tutafungua shule mwezi machi.  (Our school opens in march.)
 Ndege kuondoka saa tatu asubuhi . ( The plane leaves at 9am)
E: Hutumika pamoja na future tense (wakati ujao) kuelezea matukio huandikwa kabla baada ya neno WHEN, UNTIL, AFTER, BEFORE, na AS SOON AS.
Mfano:  Nitakuja wakati mama yangu atakaposema sawa.  ( I will come when my mother says it is ok.)
Mara tuu atakapofika, tutafungua sherehe.  ( As soon as she arrives, we will open the party.)
F: Kuna vitendo katika Present Continuous havitumii ING hivyo inabidi sentensi yako ya Present continuous iwe katika Simple Present. Tulijifunza hili katika somo lililopita. Kama hukusoma tafadhali BOFYAhapa usome.
Mfano: Kwa present continuous tense hauwezi kusema:
I am hearing a lot of noise. ( Ninasikia makele )
She is  trusting you now.  ( Yeye anakuamini)
He is understanding you now. ( Yeye anakuelewa sasa)
I am promising to pay you. ( Naahidi kukulipa)
Badala yake sentensi hizo zinatakiwa kuwa katika simple present tense hivyo twaweza kuwa na:-
I hear  a lot of noise
She trusts you
He understands you
I promise to pay you. 
Share:

HII KALI: MTANZANIA ADAIWA KUMPA VITISHO MKE WA RAISI ZUMA


KAMA HAUKUJUA BASI JUA KUWA
Mtanzania aitwaye Stephen Ongolo anashikiriwa na polisi huko Afrika Kusini kwa kosa la kumpa vitisho mke wa raisi Jackob Zuma.
Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa jana na News24.com ni kwamba mtanzania huyo anadaiwa kumlazimisha mke wa raisi Zuma kumpa fedha Rand laki mbili ili asitoe siri za mke huyo wa raisi.
Hata hivyo, bwana Ongola amekanusha kumtisha mke wa raisi.

Soma zaidi habari hii toka news24.com
Share:

KWA MUONGOZO HUU HATA WEWE WAWEZA ANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA


Unapotaka kujifunza kitu au mada husika ni vema ukaelewa kwanza maana ya kichwa cha habari, na mantiki ya kitu husika kuitwa hivyo kiitwavyo. 
Kuelewa huko kutakuwezesha kuelewa zaidi yale utakayosoma ndani ya mada husika, na hata mpangilio wa kitu husika.
Nikupe mfano: MCHANGANUO WA BIASHARA.
Hapa kuna maneno mawili -mchanganuo na neno Biashara.
Elewa kuwa kitu kilicho changanuliwa maana yake ni kuwa kimefafanuliwa kwa vipande vidogo vidogo ili kukupa uelewa wa jinsi kilivyo hivyo kilivyo kizima.
Neno biashara ni shughuli yeyote inayolenga kuleta faida.
Hivyo ukiunganisha maneno hayo mawili yaani Mchanganuo , na Biashara, unapata kujua kuwa basi Mchanganuo wa biashara itakuwa ni maelezo ya kina jinsi biashara biashara husika imeundwa.
--Kwa kufikiria hivyo haraka haraka tuu unajua basi mchanguo wa biashara ili kweli ukupatie hiyo picha kamili ya biashara - hivyo lazima tuifafanue biashara katika visehemu vyake vidogo vidogo kama vile, je biashara husika inahusu nini, nani ni wateja wa hiyo biashara, kwanini hao ni wateja wa hiyo biashara, ielezwe wazi bei za bidhaa husika, kiwango cha mauzo walau kiwa wiki, kwa mwezi, kwa mwaka, na hata miaka 3. 
Ielezwe wazi wazi mapato yatakuwa yapi katika tshs., kwa mwezi, mwaka n.k
Ielezwe vema gharama ni zipi, na ni kiasi gani katika tshs. Pia tujue wazi ni kwa mwezi, mwaka, n.k
Ielezwe usimamizi wa biashara utakuwa wa aina gani, nani atafanya shughuli zipi na atawajibika kwa nani.
Taarifa za fedha za mwezi, mwaka na miaka kadhaa kama 3 hivi zifafanue muonekane wa kifedha wa biashara husika.
Pia ielezwe changamoto zinazotegemewa kuikumba biashara na pia maandalizi yaliyopo kukabiliana na hizo changamoto.
--Si umeona? Ukisoma maelezo hayo yote yanakupa kweli picha nzima ya biashara lakini katika vipande vidogo vidogo. Kwa jinsi utakavyochambua unaondoa mashaka yoyote ya mtu kusema haielewi kitu kuhusu biashara husika. Mfano hauwezi tuu kusema unataraji kupata mapato kila mwezi laki 2, bila kuchambua hiyo laki mbili itapatikanaje.
Share:

FAHAMU JINSI YA KUANZA KUTIMIZA NDOTO YAKO HATA KAMA UNADHANI NI NGUMU


Kinachofanya watu wafanikiwe ukiacha bahati ni swala la kujituma katika wayafanyayo. Haitoshi tuu kuota na kutamani kuwa wa aina fulani, haitoshi tuu kuwa na mipango na mikakati isiyo na utekelezaji.

Wengi hupenda kuwa watu wa visingizio yaani kutoa sababu ya kwanini hawafanyi watakiwayo kufanya au kwanini hawajawa vile wanavyotamani kuwa. Mara nyingi sababu wazitoazo ni wazi kuwa hazitaji kwamba wao pia wanahusika na hali waliyonayo. Mara nyingi visingizio ni watu wengine kuwakwamisha, au mazingira.

Ukitaka mabadiliko siku zote fikiria kwamba sawa pamoja na yote unayoyaona kuwa ni magumu, je wewe kweli nini unaweza kufanya, hata kama ni kidogo.

Pengine tatizo ni namna ya tabia yako ilivyo, pengine ni majivuno yako na kujiona wa thamani zaidi au haufai kukabiliana na changamoto. Pengine ni kwakuwa haupo tayari kusamehe, au kuendana na watu fulani ili mambo yaende sawa. Pengine unahitaji ka uvumilivu kadogo tuu ili mambo yako yaende sawa.
Kanuni rahisi ya kukumbuka katika kuwajibika na kuepukana kuwa mtu wa sababu ni kuamini kuwa lengo lako ni la msingi zaidi kuliko hayo yanayokukwamisha. Anza sasa kuweka mbele ndoto yako na usikubali mtu au mazingira yakufanye urudi nyuma.

Usikubali watu-wasemayo au tabia zao ziwe kikwazo cha ndoto yako kwani hayo ni mawazo yao, kumbuka hata wewe una mawazo ambayo wengine hawawezi kuyabadilisha. Usikubali kuweka mtazamo wa mtu mwingine mbele au unayodhani anawaza juu yako mbele kuliko ndoto yako yenye thamani zaidi.

Kuhusu mazingira, kama huwezi kubadili mazingira uliyopo basi vumilia na thaminisha kuwa ni ndoto yako ni bora zaidi kuliko kuwa mnyonge wa mazingira. Ukifikira zaidi utaona mazingira hayo magumu yanakupa fursa.
Share:

HII NDIO MAANA HALISI YA KUENDESHA BIASHARA KISOMI

Kwanza kabla hatujaenda mbali tambua yafuatayo:
  • Sio lazima mwenye biashara awe msomi ili biashara iendeshwe kisomi
  • Sio kila msomi anaweza endesha biashara kisomi.
  • Kuendesha biashara kisomi sio tuu kufanikisha biashara ipate faida.
  • Kuendesha biashara kisomi ni zaidi ya elimu ya darasani ya biashara

Endelea kusoma ufahamu vizuri nini cha kufanya ili biashara iendeshwe kisomi.
Ipo hivi,  kuendesha biashara kisomi ni pale unapoamini na kutenda mambo yahusuyo biashara yako kwa imani na mtazamo kuwa biashara yako ipo sio tuu kwa sababu ya kupata faida ili wewe ujinufaishe bali huko kupata faida ni sehemu tuu ya malipo yako ya kukufanya uihudumie biashara yako ifikie kile ambacho kweli haswa ndio lengo lake.
Hivyo kwa mtazamo wa kisomi ni kuwa pamoja na kwamba wewe unajiita bosi, kiukweli wewe ni mtumishi tuu wa hiyo biashara. 
Itazame biashara yako kama kiumbe ambacho kimekwisha zaliwa, kinahitaji kuishi kwa miaka mingi iwezekanavyo. Hata hivyo chukulia binadamu pia kama anaishi tuu ili mradi kukuche, haipendezi. Ndivyo kwa biashara pia. Unahitaji kuikuza, unahitaji kuifanya ionekane na yenywe ya muhimu. Unahitaji kuilinda dhidi ya majanga, na pale inapoumwa (kukosa wateja, au changamoto nyingine za biashara) wewe kama mzazi wake unatakiwa kuisaidia kurudi kwenye afya njema na pia kuikinga isipate matatizo tena.
Hata hivyo wapo pia wazazi wanaozaa watoto wakawatelekeza, wapo wazazi ambao wanazaa watoto ili mradi tuu na wao waseme wana watoto , lakini mpango wa kuwafanya hao watoto wawe kweli wenye kufanya mambo ya msingi kimaisha hawana. Watoto wanaishia kuishi maisha magumu, wengine wanaishia kuuawa kwa wizi. 
Hapa tatizo ni mpango-toka mwanzo mzazi hakuainisha nini anataka kufanya kwa ajili ya mtoto wake ( Utasema kila mzazi anamtakia mema mtoto wake, ni kweli, ila neno mema ni neno pana sana. Na pia kutamani sio kutenda). Wakati mtoto anakua, ni jukumu la mzazi kumchunguza mtoto na kumuandalia mazingira ya kuwa mtu bora. Ndivyo kwenye biashara pia, tumesema ichukulie biashara yako kama kiumbe. 
Jiulize maswali haya:-
1. Je, ni jambo gani haswa la msingi biashara yako inafanya hapa duniani : 
Biashara zote tunazosema zinaendeshwa kisomi ni kuwa zimejifafanua wazi kuwa zipo kutatua tatizo fulani. Zimejifafanua vema ni kwa namna gani zitatatua tatizo hilo. Na vipi zinataka kujulikana katika ulimwengu huu. Maelezo haya ya kusudio la biashara na muelekeo wake  hutajwa katika kitu kinachoitwa MISSION na VISION.
Unakumbuka nilitaja hapo mwanzo kuwa kupata faida sio lazima iwe ndio dalili ya kuendesha biashara kisomi. Ni kweli, wengine wanapata faida kwa dhuluma, kwa hongo, na hata kwa kukandamiza wengine. Kiukweli wengine hawana hata bidhaa kweli halisi wanayozalisha na itakayokuwa endelevu. Ni swala tuu la muda kwamba ni kipindi chao cha “kutesa” au ni kwa sababu ndio wamejikuta wapo kwenye mtandao unaowafanya wawe hapo walipo.
Hii inatuleta kwenye pointi ya pili: 
2. Biashara ya kisomi ina mpango kuifanya biashara iwe endelevu.

Mipango na mikakati ya mara kwa mara inafanywa ili kuifanya biashara iweze kujiendesha, iwe kukua na pia isiwe tegemezi kwa maamuzi yasiyo ya kitaalamu. Kufanya biashara endelevu ni pamoja na kuhakikisha kuwa biashara ina akiba ya kutosha, ina uongozi wenye kuelewa biashara inaendeshwaje, na kuthamini utaalamu. 
Nakumbuka tuliwahi kuanzisha biashara na jamaa kadhaa ilikuwa ni wasomi tupu toka UDSM na kweli kwa simu za mwanzo tulipata fedha hata hivyo hatukuwa na mipango endelevu na uongozi wenye kuheshimu biashara. Ilikuwa ili mradi tuu tupate hela tugawane siku ziende. Najua bado zipo biashara nyingi za namna hii zipo ndogo vile vile au zinakaribia kufa. Au la zinaleta presha tuu kwa wamiliki. 

3. Biashara inayoendeshwa kisomi imemuweka mteja kwanza: 
Mteja ndio haswa bosi wa kweli kwani yeyé anaweza kumwachisha kazi hata mmiliki wa biashara (Subiri biashara yako ikose wateja uone kama hautofunga). Hivyo biashara ya kisomi ili ibaki kuwa endelevu inabidi itumie muda wa kutosha kujifunza tabia, mahitaji na uwezo wa wateja katika kununua bidhaa. Inahitaji pia kujenga mahusiano bora, na zaidi sana kuwa na mbinu za kufikia wateja wapya zaidi na zaidi.
Biashara inayoendeshwa kisomi inazingatia kuwa na bidhaa sahihi:  Ndio ukweli ulivyo, kwamba ili wateja waendelee kukuajiri inabidi uwe na kitu sahihi cha kutatua mahitaji yako. Hivyo basi ni muhimu kuwa na bidhaa yenye kutimiza mahitaji ya wateja wako. Na kama alivyowahi kusemaKumbuka maneno haya ya Seth Godin, gwiji wa marketing :
"Quality doesn't mean perfection. It means keeping the promise the customer wants you to keep. "
Yaani: 
 Ubora wa bidhaa hauna maana utengeneze kitu kisicho na mapungufu , bali ina maanisha kuwa utimize ahadi ambayo mteja anataka uitimize.
4. Biashara inayoendeshwa kisomi inazingatia kuwa na usimamizi ulio imara: 
Usimamizi imara hapa unaanza kwanza kwenye ujuzi wa bidhaa husika inayozalishwa au kuuzwa, pia ujuzi wa mambo mengine ya msingi kama vile usimamizi wa fedha, usimamizi wa wafanyakazi, mawasiliano sanifu,  ujuzi wa masoko,  uwezo wa kuweka mipango, kodi, na ujuzi wa kusoma mazingira na mabadiliko katika jamii ili kuweza kuendana na mabadiliko. Sio lazima mmiliki wa biashara ajue yote haya, ila anaweza kuajiri watu wenye ujuzi wa mambo husika wamsaidie.
Share:

UKWELI KUHUSU UGUNDUZI WA ISAACK NEWTON NA KUANGUKIWA NA TUNDA

Kuna hadithi maarufu ya mwanasayansi maarufu Sir Isaack Newton, isemayo kuwa akiwa amekaa siku moja chini ya mti alidondokewa na tunda aina ya Apple, akaamua kulirusha tena juu ila Apple hilo likarudi chini.  Ndipo katika kujiuliza uliza sana akapata jibu kujua kumbe ni kwa sababu ya nguvu ya mvutano ya dunia. Ingawa ukweli wa hadithi kwa mujibu wa Newscientist.com ni kwamba Sir Isaack Newton hakudondokewa na tunda hilo, kwani katika historia ya maisha yake, moja ya mambo aliyomueleza mwandishi maalum aliyeandika historia yake ni kuwa yeyé Isaack alikuwa tuu akipita shambani na akashuhudia tunda hilo likianguka, alijiuliza maswali hayo kisha akagundua hicho alichogundua.

Ugunduzi mwingi umefanywa kwa mtindo huo, tafuta hata kujua jinsi kanuni ya Paisagorasi (Pythagoras theory) ile kanuni maarufu ihusuyo pembe tatu.

Lengo la kukudokeza hadithi hizi ni kukumbusha umuhimu wa wewe pia kuwa mtazamaji wa mazingira, kujifunza mambo yanavyobadilika, kisha kuwa na mtazamo mpya. Wengi bado wanaamini yale yale waliyokariri toka babu na babu bila hata kuhoji. Aina ile ile ya msosi, kuvaa, jinsi ya kugharamia maisha yao n.k. 
Sio lazima uwe unataka kugundua kitu, ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kujiuliza uliza kuhusu mambo, kuwa mtazamaji makini, na kukusanya taarifa ili kuunganisha mambo ni muhimu hata kwako ili uweze kujikwamua kutoka katika utumwa wa kifikra. Jifunze mambo mengi sio kwa sababu tuu unataka kumeza kama yalivyo, bali tafakari zaidi na ulinganishe mambo yanavyoenda. Ulichoamini jana pengine sio sahihi leo.

Nikuache na maneno haya

Anthony Robbinson: 

“If you do what you've always done, you'll get what you've always gotten. ”“Kama utafanya yale yale ambayo umekuwa ukifanya siku zote, utapata yale yale ambayo siku zote umepata”

Albert Einstein:

“Imagination is more important than knowledge. For knowledge is limited to all we now know and understand.”“ Kufikiria kwa kujenga ufahamu mpya ni muhimu Zaidi kuliko ufahamu. Kwakuwa ufahamu una kikomo kwa yale ambayo tunajua na kuyaelewa sasa.” 
Share:

JIFUNZE KIINGEREZA SOMO LA 3: ADVANCED PRESENT CONTINOUS TENSE

Kaitka somo la leo tunajifunza mambo mengine ya msingi katika Present Continous tense.
Somo hili ni muendelezo wa somo lililopita. Kama haukusoma tafadhali bofya hapa kusoma.

VITENDO MAALUM VISIVYOTUMIA ING
Umejifunza kuwa ili kutunga sentensi katika present continous ni lazima vitendo viwe katika ING, mfano He is drinking, We are going to school, n.k
Hata hivyo kuna vitendo ambavyo hautakiwi kutumia ING. Mfano wa vitendo hivyo ni:
  • Love (Penda):  Ni makosa kusema I am loving you now. Sema  I love you.
  • Hear (Sikia):  Sio I am hearing you. Ila sema I HEAR you now.
  •  See (Ona):  Sio We are seeing them. Ila sema  We SEE them. ( Tunawaona)
  • Need (Hitaji): Sio We are needing it now. Ila sema We NEED it now. (Tunakihitaji sasa)
  • Want (Kutaka kitu). Sio She is wanting ugali. Ila sema She WANTS ugali. (Yeye anataka ugali)
  • Like (Kupenda). Sio I am liking it. Ila sema I LIKE it.
  • Know (Fahamu). Sio  She is knowing a lot. Ila sema She  KNOWS a lot . ( Yeye anafahamu mengi)
  • Remember (Kumbuka). Sio I am remembering now. Ila sema I REMEMBER now. (Ninakumbuka sasa)
  • Understand (elewa): Sio I am understanding you . Ila sema I UNDERSTAND you. (Ninakuelewa)

Hivyo kumbuka kuwa kwa vitendo hivi Love, Hear, See, Need , Want, Like, Know, Remember , na Undersand huwa tunatumia PRESENT SIMPLE TENSE hata kama matendo husika yanahusu PRESENT CONTIONUS TENSE.
Vitendo vingine vinavyofuata sheria hiyo hapo juu niliyoeleza ni want, cost, own, care, contain, owe, possess, seem, belong na exist, 

Katika somo litakalofuata utajifunza Zaidi kuhusu PRESENT SIMPLE TENSE.

VERB TO BE
Jinsi ya kuelezea namna watu au vitu vilivyo: ( TO BE), na ili kuelezea hali kwa mfano:-
Huyu ni mgonjwa
Yule ni mzima
Sisi tunafuraha
Unahitaji kujua namna ya kutumia Verb To (Yaani AM, IS na ARE) kwa wakati uliopo hali ya kuendelea.
Umeshasoma jinsi ya kutumia AM, IS na ARE ila kumbuka ulijifunza kutumia hizo AM, IS  na ARE pamoja na vitendo mfano ulijifunza kusema HE  IS READING (Anasoma), WE ARE NOT COMING (Sisi hatuji).
Ni vema ukajua utofauti wa IS, ARE, AM kama verb to be, na  wakati ambapo tunazitumia kuunganisha na vitendo. Umeona kuwa IS, ARE , AM zikitumika na vitendo lazima vitendo viwe na ING, mfano He IS reading.
Hata hivyo tunapozungumza IS , ARE , na AM kama Verb To, hapa hatuhusishi vitendo. Mfano
He is fine ( Yaani muda huu yeye yupo poa) Hapa mbele ya IS hakuna kitendo.
We are happy now. ( Muda huu, sisi tuna furaha). Hapa mbele ya ARE hakuna kitendo.

ACTIVE VOICE and PASSIVE VOICE:
Unapotunga sentensi una uchaguzi wa kuanza na mtendaji wa tendo kama vile

John anaandika barua.( John is writing a letter)- Hapa mtendaji ni John, na anachokitenda ni BARUA.
Mtindo huu wa kuanza na mtenda wa tukio , tunaita ACTIVE VOICE.

Hata hivyo unaweza pia kuamua kuanza na Mtendwa, mfano:
Barua inaandikwa na John ( A letter is being written by John).
Wao wanafundishwa na Issa( They are being taught by Issa).
Mtindo huu wa kuanza na mtendwa wa tukio , tunaita PASSIVE VOICE

Umegundua nini ?
Ni kwamba kama unaanza na mtendewa wa tendo basi ni lazima utumie neno BEING, halafu kitendo kibadilishwe kiwe katika mtindo tuuitao Past Participle. 
Mfano:
WRITE inakuwa WRITTEN,  
Teach inakuwa TAUGHT n.k. 

Kujua past participle za vitendo vingine Zaidi.  

Tafadhali BOFYA HAPA kudownload hapa orodha ya vitendo na past participle zake
Share: