UTAPENDA KUSOMA STATUS HIZI 10 ZA FACEBOOK

Ndio, Facebook ni sehemu ambayo unaweza kuburudika na pia kujifunza mambo kadhaa ya kimaisha. Nakualika upitie status hizi za Facebook ujifunze kitu:-

Status 1:
Find X, in :- X+Y=18, given that Y=5.
Hapo GIVEN imerahisisha kazi.
Ingekuwa hivi hata ktk maisha kwani kuna vitu vingi GIVEN, ila bado tunaumiza vichwa. Mfano:-
----Ipo GIVEN kuwa: Sio kila mtu atapenda kila unachoandika hapa FB, ila mtu anaporopoka kwa kukukejeli, anakuwa "Amekuharibia Siku".
--Ipo GIVEN kuwa ni ngumu kujua ya ndani ya moyo/akili ya mtu, hata hivyo huwa tuna "maindi" pale best wetu anapotusema vibaya kwa watu wengine.

Status 2:
 Ajabu ila ni Kweli:
Mtu anataka Tanzania iendelee, pengine anaota iwe kama 'ulaya' lakini mtu huyo huyo ni mwingi wa Fitina, Majungu na Chuki kwa waTanzania wenzake wanaofanya uzalishaji/ubunifu wa kimaendeleo. Tena chuki, majungu na fitina hizo zinaelekezwa hata kwa watu wa UKOO wake!
---Ni sisi wananchi ndio wa kuleta maendeleo, serikali huweka mfumo, miundo mbinu, au mazingira bora kwa yetu.
----‪#‎MaendeleoHayaletwiNaWanasiasaPekee‬.

Status 3:
MUDA a.k.a WAKATI a.k.a TIME, ni mojawapo ya sababu kubwa ya utofauti wa viwango vya ubora wa maisha tulivyonavyo.
Wengine kila wiki au kila mwezi ukiacha kuingiza "Mshiko" wameingiza ufahamu fulani mpya, ufahamu wenye maana.Sio tuu wanawaza, bali wanaongeza uwezo wao wa baadae wa Ufanisi.
Ila kibongo bongo, wengi mpango mzima ni "mshiko" kwanza kwa sasa, kwa mbinu zile zile zisizobadilika+kucopy & paste.
Niingize kidhungu: I think TIME should be recognized as an Element of Production.
‪#‎Hatua3mbele5nyuma‬

Status 4:
Jambo La Kushare leo kuhusu AMERICA:
Nilipokuwa Afrika, hususani Tanzania tulizoea kuwaita watu toka USA kuwa ndio WAMAREKANI - yaani watu wa AMERICA.
Hata hivyo ukiwa bara la America wamarekani wanatambulika kama watu toka UNITED STATES, full stop. Kwani hata wa brazil nao ni waAMERICA, hata waColombia nao ni WaAMERICA.
--Hivyo kibusara mtu toka U.S.A hujitambulisha kuwa " I am from united States". Hamalizii lile neno AMERICA kwani watamshushua kuwa hata wao ni Wa AMERICA.

Status 5:
Mojawapo ya tatizo kubwa katika jamii zetu ni UGUMU WA WATU KUACHA WALIYOJIFUNZA, sio KUJIFUNZA MAPYA.
“The first problem for us all, men and women, is not to learn, but to unlearn.”
Gloria Steinem

Status 6:
There is really too little we can do Without Sacrifice.
Great things require great sacrifices.
Mambo Mengi ya Msingi Yanataka kujinyima, kutoa kafara !

Status 7:
One day, your ship will come in. Maybe it already has. But you will breakthrough and earn the money - and likely more - than you've always wanted. This will bring you many benefits, but a few problems as well, particularly in the form of negative reactions from others. No one will ever know how hard you worked to get where you are. No one will ever understand the sacrifices you made. It's not worth trying to explain.
----Craig Ballantyne

Status 8:
 KWA WENZANGU NA MIE MNAOJAZA ALAMA ZA RELI (#) KWENYE STATUS ZENU:
Kwa usahihi, alama ya # hutumika kuifanya status iingie katika kundi maalum la aina ya status. Mfano kama utaweka ‪#‎Majanga‬, basi unailazimisha status yako iingizwe katika kundi la status zinazotumia hiyo alama ya Majanga. Hii ina maana kuwa kama kuna watu wengine wametumia hiyo alama ya #Majanga, basi nyote status zenu zitaorodheshwa huko.

Status 9:

Mafanikio ya mtu yana mahusiano makubwa na ya moja kwa moja na namna anavyofikiri kuhusu makosa. Mfano kama umetia juhudi hasa za kutosha katika jambo kisha halikuwa vile ulivyotegemea, basi ujue huko si kushindwa, unajiweka sawa, wakati mwingine utaweza. Usiangalie nani alitegemea ufanye nini, wewe unajua uwezo wako ulipoishia, na dhamira yako ilivyokuwa safi katika hilo ulilolifanya. Unapojipa nafasi za kujaribu bila kuogopa kushindwa, na unapochukulia ushindi kama sehemu tuu ya maisha na mwanzo wa changamoto zingine, basi unajiweka vema kuwa 'mpiganaji' hodari na mtu mwenye mafanikio endelevu.
Tafakari....... Chukua Hatua.

Status 10:
Kipimo sahihi cha Maendeleo au Mafanikio yako sio kujilinganisha na wengine kwani siku zote watakuwepo watu waliokuzidi na unaowazidi. La Msingi ni kupima namna gani ulichonacho kinakusaidia kutimiza mahitaji na kukuweza kuuishi UBINADAMU wa kweli. Pengine, ukicheki ulivyoyapata hayo mafanikio waweza jisuta au kujipongeza vizuri !
N:B: Status hizo hapo juu ni kutoka kwa Facebook Profile yangu.
John.
Share:

JINSI YA KUWASAIDIA WATOTO WAJE KUWA WAJASIRIAMALI

Wajasiriamali ni watu muhimu sana katika jamii, kwa sababu nyingi kama vile kuongeza ajira, kuongeza bidhaa na huduma, kuboresha maisha ya watu kupitia bidhaa na ajira n.k. Mjasiriamali  ni mtu mwenye kuthubutu kuanzisha shughuli ya uzalishaji, kuboresha utendaji wa namna fulani. Wajasiriamali huamini katika 'ndoto' zao , na hukubali kujishughulisha kwa shughuli zozote wanazodhani zitapelekea 'ndoto' zao kufanikiwa, huku wakiamini pia kuna uwezekano wa wanayoyafanya yasifanikiwe. Hata hivyo hatari hiyo ya kutokufanikiwa, haiwafanyi kuacha wanayolazimika kufanya.
Makala hii inadokeza mambo unayoweza kufanya kwa ajili ya mtoto ili kumuandaa mtoto kuja kuwa mjasiriamali.
1. Kujifunza 'kutengeneza' fedha: Msaidiie mtoto kadri anavyokua na kupata ufahamu wa kutosha awe na utamaduni wa kujiingizia kipato. Mfano unaweza kumpa kazi ambazo akifanya kwa kiwango mnachokubaliana unamlipa fedha. Muweze pia kushiriki shughuli ndogo ndogo za ujasiriamali kama vile kukaa dukani (kama mna duka), kupeleka bidhaa kwa wateja wako, n.k  Hii itamsaidia kujenga ufahamu kuwa fedha inapatikana kwa mabadilishano ya bidhaa/huduma na ataanza mapema kujenga ufahamu wa mbinu, matatizo na michakato ya kijasiriamali. Pengine vinaweza visimsaidie sana akiwa mtoto, ila kadri anavyokuwa, ataweza kuunganisha 'uzoefu' wake.

2.Nidhamu ya fedha: Mtoto anapaswa kuelimishwa kuhusu matumizi ya fedha, ajue na kuweka akiba. Pia kwa nidhamu ya fedha, inapasa mtoto asizoeshwe kupewa fedha kirahisi rahisi, kwani hii haimjengi kufikiria kuhusu 'kutengeneza' fedha, badala yake anazoea 'kudaka', hivyo kumuandaa kuwa muajiriwa wa kudumu.

3. Ulimwengu wa biashara: Ni vizuri kumpatia mtoto ufahamu wa mambo yanavyoenda katika ulimwengu wa biashara, mfano aone vile unavyojadili bei, ajifunze kuhusu huduma kwa wateja, na unapoona hayo unakuwa unampa maelekezo mtoto. Mfano, unapokuwa naye na ukapatiwa huduma mbaya toka kwa mfanyabiashara fulani, mueleze mtoto kuwa hivyo sivyo sahihi katika ulimwengu wa biashara. Muweze mtoto kutembelea maeneo ya uzalishaji kama vile viwandani.
We are what we repeatedly do.- Aristotle
Sisi huwa vile ambavyo mara nyingi tumezoea kufanya.
4. Chochea ubunifu wake: Watoto karibu wote wana aina fulani za ubunifu. Msome mtoto wako, na mpe moyo kwa kila jambo analofanya la ubunifu. Mfanye atambue kuwa unamuamini, na pia mueleze kuwa anaweza kufanya lolote analodhani anataka kufanya la kiubunifu. Msaidie ikibidi kununua vifaa, kumpeleka safari mbalimbali, n.k ili mradi awe huru kubuni. Hapa unamjengea uwezo wa kujiamini.
Imagination is more important than knowledge.-Albert Einstein
Kufikiria/mawazo ni bora kuliko ufahamu
5. Mawasiliano na mtoto: Watoto wanatabia ya kuamini zaidi wazazi au walezi wao. Hivyo una nafasi kubwa ya kumjenga mtoto kuwa mjasiriamali kwa kufanya nae mazungumzo ya mara kwa mara. Mfundishe kuwa na mikakati. Muulize anapenda kufanya nini, muulize anapanga kufanya nini katika muda wake wa mapumziko, n.k. Pamoja na ugumu wa maisha unaowafanya wazazi na walezi wengi kukosa muda na watoto, hakikisha unatenga muda kwa ajili yake, kwani wewe ni mchochezi mkubwa wa namna maisha yake ya baadae yatakavyokuwa.

6. Mwezeshe kujisomea: Bila kusahau , tambua ubunifu ni nguzo kubwa katika ujasiriamali, na ili kuwa na ubunifu, mtu anapaswa kuwa na taarifa /ufahamu mkubwa wa mambo kwani ufahamu huo ndio unamuwezesha kutambua yapi yanawezekana na yapi hayawezekana, na hapo ndipo anapokuja kuona 'gap' iliyopo ili kuziba hiyo 'gap'.
Hivyo basi , mjengee mtoto mazoea ya kujisomea. Muwezeshe ajue lugha vema hususani lugha ya kiingereza.

Hitimisho:
Haijalishi aina gani ya fani mtoto atakuja kufanya kazi hapo baadae, awe mwanamichezo, mwanasheria, mhandisi, mhasibu, daktari , n.k, uwezo wa kufikiria kijasiriamali, uwezo wa kutaka kuzalisha zaidi, ni muhimu kwake na kwa jamii. Na zaidi sana, ajira atakayopata hapo baadae itamsaidia kujiingizia kipato ambacho kitamuwezesha kukusanya mtaji wa kujiajiri.
Kuna msemo mzuri toka kwa Peter F. Drucker:
“This defines entrepreneur and entrepreneurship - the entrepreneur always searches for change, responds to it, and exploits it as an opportunity.”
Hivyo kumsaidia mtoto kuwa mjasiriamali kuna faida kubwa zaidi kuliko kumuacha hivyohivyo. Anza sasa.
Share:

TATUA TATIZO HILI LA FACEBOOK

Je, Unasumbuliwa na MESSAGE usizozitaka kuziona, hususani toka kwa watu usiowajua ?
Nenda sehemu ya Settings, kisha chagua kuwa Unataka kupokea message za Walio FRIENDS zako tuu.
Message nyingine zote zitaingia kama SPAM, hivyo hazitokuja INBOX yako. Zitapelekwa kwa Folder maalum la SPAM, ni mpaka ulitafute hilo folder la Spam ndio utaziona message nyingine kama hizo za kukusumbua.

Kama unataka kuangalia Messages ambazo zimeingizwa kwenye folder la SPAM, unachotakiwa kufanya ni kuenda sehemu ya MESSAGE (Kushoto mwa profile yako),  kisha bofya hapo juu kama unavyoona kwenye picha hapa chini.
Unaweza kufanya hivi, kwani pengine kuna mtu muhimu ambaye si Friend wako amekutumia message ambayo ungependa kuisoma.

Kwa hisani ya MBUKE TIMES Teknolojia

Share: